Wikend

DAKIKA 184 BILA YA KUONA NYAVU WASHAMBULIAJI WA YANGA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdbpcztXRyVH0oXWfrbOwy-jNPdWJ6d1ELYY87DEMk53xPUuGrJJWqASro7LWxc2adbgdcR_4yDB4rqOflEKOcxQOUnh2MwaVSG1EFU3V07NyOeGTxzhSkslU1QIpCp9n4bNxK-wLxSJ70/s1600/SSERUNKUMA+NA+NDANDA.JPG
Wikiend iliyopita imeshuhudia muendelezo wa ligi kuu ya vodacom, ligi daraja la kwanza Tanzania bara sambamba na kombe la taifa kwa soka la wanawake.

Kipengele hiki kinakuletea mjumuisho wa matukio ya kimichezo yaliyojiri mwishoni mwa juma lililopita na dawati la sports in bongo kufanikiwa kuyanasa.

MATUKIO KWENYE NAMBA

0. HAKUNA MWENYEJI ALIYEPATA USHINDI
Si jambo la kawaida kwa timu za nyumbani kukubali kupoteza pointi katika ligi kuu ya Tanzania bara, lakini wikiend hii timu nne wenyeji za ligi kuu ya vodacom wameambulia sare ambazo ni Yanga, JKT Ruvu, Mgambo Shooting na Coastal union, huku timu tatu zikipoteza mchezo wao ambao ni Ndanda FC, Kagera Sugar na Stand united.

Kwa upande wa ligi daraja la kwanza ni wenyrji wawili ndio waliofanikiwa kupata ushindi katika michezo yao ya mwishoni mwa juma lililopita amabo ni Toto African na Geita Gold, huku timu mbili wenyeji wakipoteza michezo yao ambao ni villa squad na polis dodoma kwa mujibu wa matokeo yaliyotufikia.

1. SSEREKUMA NA DOMAYO
Kiungo wa Azam FC aliyesajiliwa akitokea yanga Franky Domayo alicheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom msimu huu baada ya kuwa nnje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 6.

Katika mchezo wake wa kwanza siku ya jumamosi alifanikiwa kufunga goli lake la kwanza akiwa na jezi za Azam FC katika ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Stand united.

Danny Sserekuma baada ya kuiwakilisha Simba SC katika michezo 9 ya ushindani jumamosi alifanikiwa kupata goli lake la kwanza katika michezo ya ushindani na likiwa ni goli lake la kwanza katika ligi kuu ya vodacom katika ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Ndanda FC.

Danny ambaye mashabiki wa yanga wamempachika jina la Mrisho Mpoto amecheza mechi 2 za ligi kuu ya vodacom, michezo 6 ya kombe la mapinduzi na mchezo wa mtani jembe.

Katika mchezo wa fainali wa kombe la mapinduzi Danny ambae ndie mfungaji bora wa ligi kuu ya Kenya msimu uliopita alifunga goli katika hatua ya kupigiana penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

2. SARE YA PILI KWA PLUIJM
Kocha wa yanga Hans van der Pluijm ameambulia sare ya pili mfululizo katika michezo wa ligi kuu ya vodacom, ambapo toka akabithiwa timu ameingoza katika michezo miwili ya ligi kuu ya vodacom bila ya kupata ushindi.

Katika michezo hiyo miwili Pluijm anae sifika kwa soka la kushambulia washambuliaji wake wamefanikiwa kufunga goli mbili na kufungwa goli 2.

Puijm alifanikiwa kuifanya yanga kuwa bora msimu uliopita na kufanikiwa kumaliza nafasi ya pili huku akiifunga goli 7 timu iliyo mlazimisha sare ya pili hapo jumamosi katika uwanja wa taifa.


3. KOCHA WA COASTAL AONJA UTAMU WA LIGI YA BARA.
Kocha mpya wa Coastal union James Nyende Nandwa ameonja utamu wa ligi kuu ya vodacom baada ya kutimiza michezo mitatu ya ligi kuu akiwa kocha wa Coastal union bila ya kupata ushindi wowote na bila ya safu yake ya ushambuliaji kupata goli lolote lile zaidi na wakiruhusu goli moja katika nyavu zao.

Nandwa ameambulia sare mbili na kufungwa mchezo mmoja katika uwanja wa CCM Mkwakwani ambapo chini ya Yusuf CHippo Coastal union haikupoteza mchezo katika uwanjwa wa Mkwakwani na walifanikiwa kukusanya point 11 katika michezo 7 ambapo alishinda michezo mitatu, na kutoa sare michezo miwili na kupoteza miwili.

5. WAWILI WAPIGWA TANO
Timu mbili zimepokea kichapo cha goli 5 mwishoni mwa juma hili ambazo ni Mtwara na JKT Kanebwa.

Timu ya wanawake ya mkoa wa Mtwara imekubali kichapo cha goli 5 toka kwa timu ya mkoa wa Ilala katika mchezo wa kombe lataifa la wanawake, ambapo juma lililo pita liliingia hatua ya pili.

Mtwara ilifungwa goli 5-0 na Ilala ambapo ni ushindi mkubwa kwa mwishoni mwajuma lililopita kwa soka la wanawake.

JKT Kanebwa walifundishwa namna ya kufunga magoli na Toto Afrika baada ya kuwachapa goli 5-2 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba hapo jana.

6. IDADI YA MAGOLI YALIYO FUNGWA.
Katika mashindano yanayo simamiwa na TFF mwishoni mwa juma ulishuhudia Ligi kuu ya vodacom kuwa ndilo shindano lililoshuhudia magoli machache zaidi baada ya kushuhudia magoli 6 tu yakitinga nyavuni.

Kati ya magoli hayo sita mawili ya lishuhidwa ya kitinga katika michezo miwili huku 4 yakishuhudiwa kutinga katika michezo miwili na kupeleka magoli hayo kushuhudiwa katika michezo minne kati ya saba iliyochezwa mwishini mwa juma lililoisha.

Simba SC ndio walioshinda magoli mengi kwa kushinda magoli 2, huku Mtibwa, JKT Ruvu, Azam FC, na Mbeya city wakifunga goli 1 kila mmoja.

Kwa mujibu wa matokeo tuliyo yapata katika ligi daraja la kwanza kumeshuhudiwa magoli 12 huku magoloi 7 yakifungwa katika mchezo kati ya JKT Kanebwa na Toto Africans.

uku katika kombe la taifa kwa soka lwanawake kukishuhuia magoli 12 huku goli 5 zikishuhudiwa katika mchezo kati ya Ilala na Mtwara.

11. DAKIKA ZILIZO ONGEZA KATIKA MCHEZO KATI YA YANGA NA RUVU SHOOTING
Katika hali isiyo ya kawaida mchezo kati ya yanga na Ruvu shooting ulishuhudia dakika 11 zikiongezwa na mwamuzi wa akiba kufidia muda uliopotea.

Katika kipindi cha kwanza ziliongezwa dakika 5 na kipindi cha pili kikaongezwa dakika 6 na kupelekea mchezo huo kuwa na dakika 11 za nyongeza na mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo mwingine ambao uliongeza dakika nyingi ni ule wa Mtibwa Sugar na JKT Ruvu ambao ulikwisha kwa sare ya goli 1-1, ziliongezwa dakika 7, dakika 5 kipindi cha pili na dakika 2 kipindi cha kwanza.

184. DAKIKA ZA YANGA BILA KUTIKISA NYAVU
Safu ya ushambuliaji ya yanga ndio safu inayo onekana kuwa bora zaidi toka kocha Pluijn na Mkwasa kukabidhiwa timu  na kufanikiwa kufunga magoli 11 katika michezo minne ya mwanzo lakini mwishoni wa juma hili wametimiza jumla ya dakika 184 bila ya kuona nyavu za wapinzani wao.

Mchezo wa mwisho kuzishuhudia nyavu za wapinzani ilikuwa ni mchezo kati ya Taifa Jang'ombe na yanga ambao ulimalizika kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililo fungwa na Andry Continho katika dakika ya 86.

Hizo ni dakika nyingi kwa yanga chini ya Pluijm kucheza bila ya kuona nyavu za mpinzani

MATUKIO BILA YA NAMBA.

MPIRA WA PASUKA
Katika uwanja wa Nangwanda ulioshuhudia mchezo kati ya Simba SC na Ndanda FC ulishuhudia mpira ukipasuka, hali ambayo baadhi ya mashabiki wa ifananisha na imani za kishirikina.

WALINDA UWANJA NA KUCHAPWA
Mashabiki wa Ndanda FC waliamua kuilinda uwanja wa Nagnwanda kwa siku mbili kabla ya mchezo dhidi ya Simba SC kwa kuhofia hujuma ambayo wangefanyiwa na Simba SC.

Pamoja na kuulinda uwanja huo walipokea kichapo cha goli 2-0 toka kwa Simba SC.

MATOKEO YA WIKIEND ILIYOKWISHA

LIGI KUU YA VODACOM

NDANDA FC 0-2 SIMBA SC
YANGA SC 0-0 RUVU SHOOTING
JKT RUVU 1-1 MTIBWA SUGAR
COASTAL UNION 0-0 POLISI MOROGORO
MGAMBO SHOOTING 0-0 T.PRISONS
STAND UNITED 0-1 AZAM FC
KAGERA SUGAR 0-1 MBEYA CITY

LIGI DARAJA LA KWANZA

VILLA SQUAD 0-1 AFRICAN SPORT
PANONE 0-0 BURKINA FASO
KIMONDO 0-0 LIPULI
MAJIMMAJI 1-1 KURUGENZI
POLISI DODOMA 0-1 MWADUI
GEITA 1-0 OLJORO JKT
TOTO AFRICANS 5-2 JKT KANEBWA

KOMBE LA TAIFA KWA SOKA LA WANAWAKE

KAGERA 1-2 MWANZA
SHINYANGA 1-0 SIMIYU
ARUSHA 1-2 TANGA
PWANI 0-0 KINONDONI
MTWARA 0-5 ILALA

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.