TFF

FIFA YATUA KUCHUNGUZA UPANGAJI WA MATOKEO

Ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) upo nchini kuchunguza tuhuma za upangaji matokeo. Waamuzi walio simamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)pamoja na watu wengine watahojiwa na ujumbe huo.

Matokeo ya uchunguzi huo yatatangazwa na Fifa baada yashughuli hiyo kukamilika.

Tunaendelea kuwa himiza wanafamilia wa mpira wa miguu wazidi kuzingatia kanuni za maadili za TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) na Fifa katika utendaji wao.

FIFA itahakikisha kuwa haki inatendeka katika uchunguzi ambao inaufanya .

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.