Kwa mujibu wa Mratibu wa mashindano hayo Mwenze Kabinda, timu zitakazocheza leo ni Kurasini Heat dhidi ya Vijana na Chang’ombe dhidi ya Prisons.
“Maandalizi ni mazuri tunaamini mzunguko huu pia utakuwa na hamasa kubwa, tunachoomba ni mashabiki wa mchezo huu kujitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange huo,” alisema Mwenze.
Alisema Jumamosi itacheza timu ya wanawake Prisons dhidi ya Jeshi Stars, JKT Stars dhidi ya Don Bosco Lioness huku timu ya wanaume ya Savio ikichuana na Pazi na Chui wakipambana na Oilers.
Katika ligi mzunguko wa kwanza uliomalizika mwishoni mwa mwaka jana, timu ya JKT ndio inayoongoza kwenye msimamo ikiwa na pointi 22 ikifuatiwa na Pazi yenye pointi 19, Mgulani 19, Jogoo 18, Savio 17, Tanzania Prisons 16, Oilers 15, Don Bosco youngstars 15, Chui na Kurasini Heat 13, na Chang’ombe inashikilia mkia ikiwa na pointi 12.
Kwa timu za wanawake inayoongoza ni JKT Stars ikiwa na pointi saba, Don Bosco Lioness pointi saba, Jeshi Stars sita, Prisons tano na Vijana Queen tano. Mwenze alisema michuano hiyo ya mzunguko wa pili ndio itakayotoa timu bora sita zitakazoshiriki michuano mikubwa itakayofanyika Mei, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment