netball

TEMEKE YAENDELEZA WALIPO ISHIA MWAKA JANA

https://24tanzania.com/wp-content/uploads/2014/01/Mary-Kajigire-300x160.jpg
MABINGWA wa netiboli msimu uliopita timu ya Temeke imeendeleza ubabe kwa kushinda mchezo wake wa tano bila kufungwa juzi katika michuano ya kuwania kombe la Taifa inayoendelea kwenye uwanja wa Sigara Chang’ombe.

Katika mchezo wa juzi Temeke iliwafunga Pwani kwa mabao 34-17 na kuendelea kuongoza katika msimamo wa michuano hiyo wakiwa na pointi 10.

Kutokana na ushindi huo iwapo itaendelea kufanya vizuri katika mchezo mmoja baada ya jana kucheza dhidi ya Dodoma itajiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao.

Timu hiyo imebakiza mchezo wake dhidi ya Tabora utakaopigwa kesho jioni. Kwa upande wa timu nyingine Mjini Magharibi ilijikuta ikipoteza mchezo wake dhidi ya Dodoma baada ya kuchapwa mabao 28 - 23.

Katika msimamo wa michuano hiyo, Mjini Magharibi inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi nane nyuma ya Temeke baada ya kushinda michezo minne na kupoteza mmoja.

Pia, timu ya Kinondoni iliifunga Tabora kwa mabao 35 - 21 na wakati huo Arusha ikiifunga Ilala kwa mabao 35-19. Timu hizo zina pointi sita kila moja, huku zikiwa zimecheza michezo minne na kupoteza mchezo mmoja.

Michuano hiyo inatarajiwa kumalizika kesho kwa timu za Tabora kuchuana na Arusha na Pwani dhidi ya Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) Anna Kibira alisema michuano hiyo imekuwa na upinzani mkali kutokana na kila timu kuwa na wachezaji wengi vijana.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.