Wikend

BAHANUZI AMKIMBIZA MAPUNDA HOSPITALINI, USHIRIKINA NDANI

MATUKIO KATIKA NAMBA

1 GOLI LA JOHN BOCCO

John Raphael Bocco amekuwa mtanzania wa kwanza kufunga goli katika michuano ya CAF ngazi ya vilabu mwaka huu, pale alipo ifungia Azam FC goli la pili dhidi ya El-merekh ya Sudan katika mchezo wa klabu binga Afrika.

Magoli mawili ya yanga katika kombe la shirikisho yalifungwa na Hamisi Tambwe raia wa Burundi, huku KMKM na Polisi wakishindwa kuziona nyavu za wapinzani wao katika michuano inayoandaliwa na CAF.

Bocco vile vile alifunga goli hilo la pili ukiwa ndio mpira wake wa kwanza kugusa toka aingie uwanjani, ikiwa ni mara ya pili anafanya tukio kama hilo.


2. USHINDI WA YANGA, AZAM FC, NA SIMBA SC

Toka msimu huu wa 2014/15 uwanze haijatokea kwa Simba SC, Azam FC na Yanga kupata matokeo yanayofanana kama ilivyotokea mwishoni mwa juma lililopita ambapo Simba SC, Yanga na Azam FC wote kwa pamoja walipata ushindi wa goli 2-0.

Simba, Yanga na Azam FC hawajafanana pekee katika idadi ya magoli yaliyoyapata mwishoni mwajuma lililopita, bali magoli yakila timu yalifungwa katika kila kipindi.

Kila timu ilipata goli lake la kwanza katika kipindi cha kwanza wakati kila timu ikifunga goli la pili katika kipiti cha pili.


4. USHINDI MNONO KWA STAND UNITED

Stand United juzi ilipata ushindi wake wa kwanza mnono toka ipande ligi kuu ya codacom, ambapo waliwafunga Mgambo shooting goli 4-1, na kupelekea mchezo huo kuwa ndio mchezo ulioshuhudia magoli mengi katika michezo ya ligi kuu ya vodacom.


5. TIMU YA TAIFA SOKA LA UFUKWENI.

Timu ya Taifa ya soka la ufukweni ikicheza mchezo wake wa kwanza wa mashindano hapo jana, walifanikiwa kuichapa timu ya taifa ya Kenya goli 5-3 katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu mataifa ya Afrika kwa soka la ufukweni.

Mchezo huo wa kwanza kwa timu ya Taifa ya soka la ufukweni ulichezwa nchini Kenya.

6. CCM KAMBARAGE

Kwa mara ya kwanza katika msimu huu wa 2014/15 uwanja wa CCM Kambarage umeshuhudia magoli 6 yakifungwa ndani ya siku mbili mfululizo, na ndio magoli mengi zaidi kushuhudiwa katika viwanja vilivyokuwa vinamichezo ya ligi kuu ya vodacom.

Mwishoni mwajuma lililopita vilishuhudia viwanja vinne vikitumika ambapo katika viawanja hivyo viwili havikushudia goli lolote likifungwa ambavyo ni CCM Mkwakwani na Nangwanda Sijaona, wakatik katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ukishuhudia magoli mawili.

Magoli hayo 6 katika uwanja wa CCM Kambarage yamefungwa na JKT Mgambo goli 1, Kagera Sugar goli 1 na Stand united goli 4.


58. BAHANUZI AMKIMBIZA HOSPITALINI IVO.

Shuti kali la mshambuliaji wa Polisi Morogoro Said Bahanuzi lilipelekea kipa wa Simba SC kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Shuti hilo la Bahanuzi lilipigwa katika dakika ya 58 ya mchezo na kumgonga Ivo Mapunda katika paji lake la uso na kupelekea kushindwa kuendelea na mchezo na kukimbizwa hospitalini.

Mapunda anaendelea vizuri japo kuwa amewekwa bandeji kwenye jisho lake moja na kupelekea kutumia jisho moja katika kuangalia.

MATUKIO NNJE YA NAMBA

KUHITIMISHWA KWA LIGI DARAJA LA KWANZA

Ligi daraja la kwanza ilifikia tamati hapo jana kwa kushuhdia michezo yote ya kundi B ikihitimishwa huku michezo ya kundi A ikiwa imechezwa siku ya ijumaa.

Timu zilizofanikiwa kupanda ligi kuu ya vodacom ni Majimaji ya Songea na African Sport ya Tanga kundi A na Kundi B ni Toto Africans ya Mwanza na Mwadui FC ya Shinyanga.


MASHABIKI WA KUNDI LA SIMBA UKAWA KUKAMATWA WAKITUHUMIWA NA USHIRIKINA.

Katika mchezo wa jana kati ya Simba SC na Polisi Morogoro mashabiki wa simba wanaojulikana kama Simba Ukawa walikamatwa baada ya kutuhumiwa kutaka kufanya ushirikina kabla ya mchezo huo kuanza.

Inadaiwa mashabiki wa Simba SC ndio waliobaini tukio hilo la Simba ukawa kutaka kufanya tukio la ushirikini ili Simba SC ipoteze mchezo huo.


MASHABIKI WAFUNGIA GETI AZAM COMPLEXS

Uwanja wa Azam complexs hapo jana iulijaza, huku mashabiki wengine wakizuiliwa kuingia kwa geti kufungwa baada ya uwanja kutapika.

Katika uwanja huo ambao jana uliweka rikodi ya kuwingiza watu wengi kulikuwa na mchezo kati ya Azam FC na El0merekh ya Sudan.

MATOKEO YALIYOTUFIKIA

MATOKEO KLABU BINGWA AFRIKA

AZAM FC 2-0 EL-MEREKH
AL-HILAL 2-0 KMKM


MATOKEO KOMBE LA SHIRIKISHO

YANGA SC 2-0 BDF XI
CF MOUNANA 5-0 POLISI ZANZIBAR


MATOKEO LIGI KUU YA TANZANIA BARA

NDANDA FC 0-9 MTIBWA SUGAR
POLISI MOROGORO 0-2 SIMBA SC
COASTAL UNION 0-0 MBEYA CITY
STAND UNITED 4-1 MGAMBO SHOOTING
KAGERA SUGAR 1-0 JKT RUVU


MATOKEO LIGI DARAJA LA KWANZA

TOTO AFRICAN 2-0 RHINO RANGER
MWADUI FC 3-1 BOKINAFASO

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.