Tanzania ilipewa wenyeji wa mashindano hayo makubwa hivi karibuni, ambapo tayari Chaneta walikubali na kupewa baraka na serikali kwa ajili ya kuanza mchakato mapema.
Akizungumza na gazeti hili jana Mwenyekiti wa Chaneta, Anna Kibira alisema mashindano hayo yatafanikiwa iwapo wadau watajitokeza kuwaunga mkono katika kufanikisha mipango.
“Tunaomba wadau mapema kwa sababu Mei sio mbali, tunataka tuanze maandalizi kuelekea kwenye michuano hiyo mikubwa kwa sababu tunaamini kuwa sisi wenyewe hatutaweza hasa ikizingatia kuwa kuna mambo mengi muhimu yatahitajika,” alisema.
Kibira alisema kwa sasa wanajipanga kuanza mchakato wa maandalizi kwani wanategemea kupata timu kuanzia 12 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Michuano hiyo imekuja ikiwa miezi michache tangu Chaneta watoke kuandaa michuano mingine ya Afrika Mashariki iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa mwishoni mwa mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment