vilabu

JULIO KUJENGA GOROFA COASTAL UNION

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg5ocp8npcecGoGj-vZQo-rbzveqVD9fXWfZ9misO6zXXGtf5TuLShyphenhyphenfag3C1ZfRKl7rV2PjXAN7TQgOuSJQ2ASHd6NRaG7CwQjgcdOd87-0T-SUzaEdJAvDJxQyuUNbBdkQnTilK_OerNG/s1600/julio+look.JPG
Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo Julio leo ameonekana katika mazoezi ya Coastal union, ambayo imemchukuwa kama kocha msaidizi wa timu hiyo, akimsaidia kocha  toka Kenya James Nandwi.

Julio akizungumza baada ya mazoezi ya coastal union amesema kuwa amekuja kutimiza ahadi aliyoitoa wakati kikosi chake cha Mwadui kilipo cheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal union.

"Wakati tumekuja kwenye mechi ya kirafiki kati ya timu yangu Mwadui FC na coastal union tulikubaliana, nikimaliza tu, mijekuweza kuwasaidia kufikia malengo, sasa nimekuja kufanya lile nililo ahidi kwa sababu mie ni mtu nilikamilika akili na nasema nimukaja kufanya kile tulicho kisudia na sasa na kuendelea coast itatisha," alisema Julio.

Julio ambaye anasifika kwa kauli anazotoa, aliongeza kuwa yeye ni kama Konoike ambao ni wajapana na wachina wanaofanya ujenzi wa madaraja na majumba makubwa.

Julio alisema kuwa amemaliza kujenga Daraja Shinyanga na sasa ni zamu ya kujenga gorofa Tanga.

Mchezo wa kwanza kwa Julio katika kiti cha usaidizi ndani ya coastal union ni dhidi ya Mgambo shooting siku ya jumamosi hii (februari 28).

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.