MATUKIO KATIKA NAMBA
1. WENYEJI WAPATA GOLI MOJA ISIPOKUWA AZAM FC
Mwishoni mwa juma lililoisha timu wenyeji katika ligi kuu ya vodacom wamepata kufunga goli 1 isipokuwa Azam FC, ambaye hakupata kufunga goli lolote lile.Wenyeji pia waliofunga goli 1 walipata ushindi isipokuwa Mbeya city ambayo ilifungwa goli 3, wakti wenyeji wengine wakitoka bila nyavu zao kuguswa.
2. KADI NYEKUNDU KWA STAND UNITED
Ndani ya dakika 12 za lalasalama wachezaji wa wili wa Stand united walizawadiwa kadi nyekundu katika mchezo uliochezwa jana dhidi ya Simba SC.Wachezaji wote hao walipewa kadi hizo baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
6. YANGA WAONDOKA NA POINTI ZOTE MBEYA
Yanga SC imekuwa timu ya kwanza kuondoka na pointi zote 6 jijini Mbeya baada ya kuichapa Tanzania Prisons goli 3-0, na wikiend iliyopita wakiwachapa Mbeya city goli 3-1.Yanga wameondoka na pointi 6 na magoli 6 ya kufunga huku wakifungwa goli 1.
Vile vile yanga imekuwa timu ya kwanza msimu huu kufikisha michezo 6 ya ligi kuu ya vodacom bila javu zao kuguswa, ambapo mchezo wa mwisho ulikuwa dhidi ya Azam FC ambapo walifungwa goli mbili, ikiwa ni kabla jana kuruhus goli jingine katika mchezo wake wa saba toka wacheze bila kuruhusu goli kwenye nyavu zao.
12. IDADI YA MAGOLI YA TANZANIA DHIDI YA KENYA
Katika majuma mawili timu ya taifa ya ufukweni imeifunga Kenya magoli 12 dhidi ya 9 na kupelekea kuingia katika hatua ya pili na ya mwisho ya kusaka nafasi ya kushiriki komba la mataifa ya Afrika kwa soka la ufukweni.608. ALLY MUSTAPHA BATHEZ
Kipa wa yanga Ally Mustapha Bathez amefikisha dakika 608 katika michezo ya ligi kuu ya vodacom kabla ya kuruhusu goli katika nyavu zake, ambapo aliruhusu katika mchezo wa jana katika dakika ya 68 goli likifungwa na Peter Mapunda.Bathez amecheza jumla ya dakika 716 katika michuano yote bila kuruhusu nyavu zake kuguswa, ambapo mara ya mwisho alifungwa na Amur Omry Janja katika michuano ya kombe la mapinduzi katika dakika ya 72.
Bathez vile vile alisimama langoni pale yanga walipo wakabili BDF XI ya Botswana katika kombe la shirikisho ambapo alimaliza dakika 90 bila ya nyavu zao kuguswa.
Bathez ameanza kuidakia yanga katika msimu huu katika michuano ya Mapinduzi, kabla ya hapo alikuwa anadaka Deo Munish Dida.
632. DAKIKA WALIZOCHEZA YNGA BILA KURUHUSU NYAVU ZAO KUGUSWA
Safu ya ulinzi ya yanga imefikisha dakika 632 katika michezo ya ligi kuu ya vodacom bila ya kuruhusu goli lolote lile.Mara ya mwisho yanga kuruhusu goli kabla ya jana ilikuwa ni zidi ya Azam FC, ambapo John Bocco alimtungua Dida katika dakika ya 66 kwa kichwa, likiwa ni goli la kusawazisha kwa Azam FC.
Baada ya yanga kucheza dakika hizo 632 jana waliruhusu goli mbele ya Mbeya city.
MWADUI WAKISHANGILIA UBINGWA WAO WA LIGI DARAJA LA KWANZA |
MATUKIO NNJE YA NAMBA
TIKETI KUWA NA VIAMBATANISHI.
Kwa lengo la kuepuka uwepo wa tiketi feki, katika mchezo kati ya yanga na Mbeya city kulishuhudia tikeiti za mchezo husika zikitolewa na viambatanishi.Viambatanishi hivto vilikuwa na vya tiketi ya mchezo kati ya Tanzania Prisons na Rhino rangers, vikiwa na muhuri wa klabu zote mbili.
WAZIMIA UWANJANI
Katika uwanja wa Kambarage kulishuhudia shabiki akipoteza fahamu, tukio lililozoeleka katika michezo inayochezwa katika uwanja wa taifa pale Simba na yanga wanapo kutana, lakini safari hii ilikuwa ni kati ya Stand united na Simba SC.MATOKEO YAMICHEZO ILIYOTUFIKIA
KUFUZU MATAIFA YA AFRIKA SOKA LA UFUKWENI
TANZANIA 7-6 KENYALIGI KUU YA VODACOM
NDANDA FC 1-0 COASTAL UNIONAZAM FC 0-0 TANZANIA PRISONS
MGAMBO SHOOTING 1-0 MTIBWA SUGAR
KAGERA SUGAR 1-0 POLISI MOROGORO
STAND UNITED 1-0 SIMBA SC
MBEYA CITY 1-3 YANGA SC
FAINALI LIGI DARAJA LA KWANZA
MWADUI FC 1-0 AFRICAN SPORTAMSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM
Rn | Timu | P | W | D | L | F | A | Gd | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | YANGA | 15 | 9 | 4 | 2 | 21 | 8 | 13 | 31 |
2 | Azam FC | 15 | 7 | 6 | 2 | 22 | 12 | 10 | 27 |
3 | KAGERA SUGAR | 16 | 6 | 6 | 4 | 13 | 11 | 2 | 24 |
4 | SIMBA SC | 15 | 4 | 8 | 3 | 15 | 12 | 3 | 20 |
5 | RUVU SHOOTING | 15 | 5 | 5 | 5 | 10 | 10 | 0 | 20 |
6 | MTIBWA SUGAR | 15 | 4 | 7 | 4 | 15 | 15 | 0 | 19 |
7 | Coastal Union | 16 | 4 | 7 | 5 | 10 | 10 | 0 | 19 |
8 | JKT RUVU | 15 | 5 | 4 | 6 | 14 | 15 | -1 | 19 |
9 | POLISI MORO | 16 | 4 | 7 | 5 | 12 | 14 | -2 | 19 |
10 | NDANDA FC | 16 | 5 | 4 | 7 | 12 | 18 | -6 | 19 |
11 | STAND UNITED | 16 | 4 | 6 | 6 | 14 | 18 | -4 | 18 |
12 | MBEYA CITY | 15 | 4 | 5 | 6 | 10 | 12 | -2 | 17 |
13 | MGAMBO SHOOTING | 14 | 5 | 2 | 7 | 8 | 15 | -7 | 17 |
14 | T. PRISONS | 15 | 1 | 9 | 5 | 10 | 15 | -5 | 12 |
0 comments:
Post a Comment