Mara ya mwisho mashindano hayo kufanyika ilikuwa ni mwaka jana nchini Uganda ambapo Tanzania iliwakilishwa na wachezaji kadhaa waliofanya vizuri wakiwamo Hilal Hilal na Sonia Tomiotto.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwaipasi alisema katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika mashindano ya mwaka huu, tayari wameshaanza mchakato wa kusaka kikosi bora.
“Tumeanza mchakato wa kuwatafuta wachezaji bora kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha, Morogoro na Dar es Salaam na tuna imani mambo yatakuwa mazuri tutakapoanza kambi baadaye,” alisema Mwaipasi.
Alisema wachezaji hao watafuatiliwa mwenendo wao katika mashindano ya kitaifa yatakayofanyika mwezi ujao, na mashindano ya wazi ya Afrika yatakayofanyika nchini Afrika Kusini.
CHANZO: HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment