Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Annie Kibira alisema kuwa kamati yao ya utendaji ilikutana hivi karibuni na kukubali kuwa wenyeji wa mashindano hayo.
Kibira alisema baada ya kukutana, walikubali kuandaa mashindano hayo Mei katika tarehe watakazozipanga baadaye.
Alisema hawajajua bajeti ya mashindano yote hayo ambayo ni makubwa kufanyika nchini. Alisema nchi shiriki zitajilipia karibu gharama zote huku waamuzi wakiletwa na Shirikisho la Kimataifa la Netiboli (INF).
Alisema kila nchi shiriki itatoa kiingilio, ambacho kitasaidia kuwagharamia waamuzi na wasimamizi wengine wa mashindano hayo. Kibira alisema wanatarajia kukutana na Serikali wakati wowote ili kuwasilisha suala hilo la kuandaa mashindano hayo ya Afrika.
Aidha, Kibira alisema Mkoa wa Shinyanga mwaka huu utaandaa mashindano ya Klabu Bingwa ya Taifa yatakayofanyika Juni.
chanzo: habaei leo
0 comments:
Post a Comment