MATUKIO KATIKA MWAKA
1 USHINDI WA KWANZA KWA YANGA TAIFA MWAKA HUU
Toka mwaka huu uingie mabingwa wa kihistoria wa Tanania Bara Yanga hawajapata kushinda katika uwanja wa taifa katika mchezo wowote wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Yamga mwaka huu wamecheza michezo miwili katika uwanja wa taifa kabla ya mchezo wa jana ambao ulikuwa wa kwanza kufunga kwa yanga katika uwanja huo mkubwa nchini.
Mchezo wa mwisho wa yanga kushinda katika uwanja huo wa Taifa ni dhidi ya Mgambo shoooting november 8 mwaka jana, ambapo alishinda goli 2-0 , baada ya mchezo huo wamecheza michezo mitatu katika uwanja wa taifa bila ya kushinda.
Yanga walitoka sare ya goli 2-2 dhidi ya Azam desemba 28 mwaka jana, wametoa sare ya bila kufungana na Ruvu shooting januari 17 na suluhu dhiri ya Ndanda FC februari mosi.
3 KAGERA SUGAR KUTUMIA VIWANJA VITATU
Kagera Sugar walianza msimu akitumia uwanja wao wa Kaitaba ambapo wamechezo michezo mitatu katika uwanja huo kabalay a kuanza kufanyiwa marekebisho katika eneo la kuchezea la uwanja huo.
Katika mchezo wake wa kwanza katika makazi yake ya matatu katika msimu huu, Kagera sugar waliibuka na ushindi wa goli 1-0.
4 MAGOLI MENGI MICHEZO MMOJA, IDADI YA TIMU ZILIZO SHINDWA KUTIKISA NYAVU
Katika magoli 13 yaliyofungwa katika michezo 7 ya ligi kuu ya vodacom, magoli 4 ndiyo ilikuwaidadi kubwa ya magoli katika mchezo mmoja, ikiwa ni sawa na idadi ya timu ambazo hazikuona nyavu mwishoni mwa juma liliopita.
Timu ambazo hazikushuhudia nyavu ni Simba SC, Coastal Union, Mtibwa Sugar na Mgambo shooting, ambapo magoli hayo 4 yamefungwa katika mchezo kati ya Polisi Morogoro na Azam Fc uliomalizika kwa sare ya goli 2-2.
5 IDADI YA SARE
Katika michezo 7 ya ligi kuu ya Tanzania bara, michezo mitano imemalizika kwa sare, huku michezo mwili ikishuhudia timu mwenyeji akiibuka na ushindi na kupelekea kukosekana kwa timu mwenyeji kupoteza mchezo.
Katika sare hizo 5 ni sare moja ambayo haikuwa na magoli ambayo ni kati ya Simba SC na Coastal union, michezo mitatu ikimalizika kwa sare ya goli 1-1 na mchezo mmoja kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
7 NAMBA ILIYOHUSIKA KWENYE GOLI LA KWANZA LA YANGA TAIFA
Saimon Msuva anae vaa jezi namba 27 alipiga krosi iliyomaliziwa na Ngassa anae vaa jezi namba 17, ambaye ndiye aliyefunga goli hilo.
Dakika 7 baada ya goli hilo Ngassa aliifungia Yanga goli la pili, ambalo lilitengenezwa na kiungo Haruna Niyonzima anae vaa jezi namba 8.
12 MICHEZO MFULULIZO TANZANIA PRISONS KUCHEZA BILA KUSHINDA
Katika michezo hiyo 12, Tanzania Prisons imetoka sare michezo 8 na kufungwa michezo minne.
MATUKIO NNJE YA NAMBA
WAUZA JEZI WAGOMA KUTOA 2000
NGASSA AKILI KUJUTA KUKATA DILI EL-MEREKHE
Dili hilo liltokea mwanzoni mwa mwaka juzi, ambapo Ngassa alikuwa kwa mkopo Simba SC aktikoea Azam FC.
Ngassa alisema kuwa aliachana na dili hilo kutokana na mapenzi yake na Yanga, na sasa anacheza kumalizia mkataba wake wa miezi mitano iliyo salia, na kuamua nini cha kufanya baada ya miezi hiyo mitano.
Ngassa alisema kuwa mwanzo walikubaliana na uongozi kumkata laki 5 kulipa deni lake, lakini cha ajabu walianza kumkata milioni na sasa ana miezi miwili ajapokea mshahara wake.
MWAMAJA AWEKWA KIKAANGONI
MATOKO YA LIGI KUU YA VODACOM
KAGERA SUGAR 1-0 MGAMBO SHOOTING
POLISI MOROGORO 2-2 AZAM FC
NDANDA FC 1-1 STAND UNITED
T.PRISONS 1-1 RUVU SHOOTING
JKT RUVU 1-1 MBEYA CITY
COASTAL UNION 0-0 SIMBA SC
0 comments:
Post a Comment