netball

ZANZIBAR KUANDAA KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLIFGQ9yAZXi0rAxuDWyy9fPndjvA6TjwDvfFI58isCiL11BhuX9Bk_XSV27XMHad4WjwoGUu8it-0zBdHjZ0c-xzRi3fZw59Ktt16JE7n-rH6eQB1tl9Ujlg81SoVPZ4UjnNMK43VQ7_v/s1600/Mke+wa+Rais,+Mama+Salma+Kikwete+akikagua+timu+ya+Tanzania.+Kushoto+ni+Mwenyekiti+wa+CHANETA,+Anna+Bayi..JPG
ZANZIBAR inatarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano ya Afrika Mashariki ya Klabu Bingwa ya mpira wa netiboli yatakayofanyika mwezi ujao.

Hayo yalielezwa na Katibu wa chama cha mchezo huo Zanzibar, Said Ali Mansab alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu michuano hiyo.

Alisema michuano hiyo itashirikisha wachezaji jinsi zote na itakuwa ikichezwa katika uwanja wa Gymkhana mjini hapa. Alisema maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo yameanza na yanaendelea vizuri.

“Mpaka sasa maandalizi yameanza kufanywa pamoja na kuongeza wigo wa kutafuta wadhamini ili waweze kutusaidia,” alisema.

Hivyo aliwaomba wadau mbali mbali wa michezo nchini kujitahidi kuwaunga mkono ili kuona mashindano hayo yanafanyika bila ya kikwazo chochote.

Nchi ambazo zinazotarajiwa kushiriki kwenye michuano hiyo ni Kenya, Uganda, Tanzania Bara pamoja na wenyeji Zanzibar, ambapo kila nchi itatoa timu ya wanawake na wanaume.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.