MATUKIO KATIKA NAMBA
1. KAGERA SUGAR WAPOTEZA KAMBARAGE
Kagera sugar imepoteza mchezo wao wa kwanza katika uwanja wa CCM Kambarage toka waanze kuutumia kama uwanja wao wanyumbani, baada ya juzi kukubali kichapo cha goli 1-0 toka kwa wenyeji wa uwanja huo Stand united.Kagera Sugar wamecheza michezo mitatu katika uwanja huo na kufanikiwa kushinda michezo yote mitatu ikiwa ni baada ya kufungwa michezo mitatu katika uwanja wa CCM Kirumba ambao walikuwa wanautumia kama uwanja wake wa nyumbani.
3. HAT TRICK YA KWANZA MSIMU HUU
Ibrahim Ajibu amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli matatu katika mchezo mmoja katika msimu huu wa ligi kuu ya vodacom, baada ya juzi kufanya hiyvyo katika ushindi wa simba wa goli 5-0.Katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ni nadra kushuhudia hat trick katika michezo ya ligi kuu ya vodacom, kwani msimu uliopita umeshuhudia hat trick mbili moja ya Amisi Tambwe alipokuwa Simba SC na myingine ni Mwegane Yeya wa Mbeya city.
5. MICHEZO MITANO BILA YA KUONA NYAVU ZA WAPINZANI
Baada ya kupata goli katika dakika ya 90 kupitia kwa Mutimba Yeya, coastal nuion wameondoa gundu la kucheza michezo mitano bila ya kupata goli.Mchezo wa mwisho kwa coastal union kupata goli ulikuwa dhidi ya Stand united uliocheza katika uwanja wa CCM Kambarage jaunari 25 na Coastal kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Coastal union juzi waliwafunga Mgambo shooting goli 1-0, ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Jamhuri Kihwelu Julio kuwa msaidizi katika benchi la Coastal union.
5. UWIANO MKUBWA WA MAGOLI KATIKA MCHEZO MMOJA
Mchezo kati ya Simba SC na Prisons umekuwa mchezo wa kwanza kuwa na uwiano mkubwa wa magoli msimu huu, kwani Simba SC waliwafunga goli 5 bila majibu Prisons.Michezo inayofuata kwa wiano mkubwa wa magoli ni mchezo katia ya Azam FC na Mtibwa sugar, Yanga na Prisons, Stand united na Mgambo shooting na Ndanda FC na Stand united ambayo yote uwiano wa magoli ulikuwa wa magoli matatu.
8. MAGOLI YALIYOFUNGWA TIMU ZA TANZANIA CAF
Mwishoni mwajuma hili timu za Tanzania katika klabu bingwa Afrika na kombe la shirikisho wamefungwa jumla ya magoli 8 katika michezo minne iliyohusisha timu za Tanzania.Mwishoni mwajuma lililopita katika kombe la shirikisho timu za Tanzania zilifunga jumla ya goli 5, yanga wakifungwa goli 2-1 na BDF XI, huku Polisi ikifungwa goli 3-1 na FC Monanan.
Katika klabu bingwa Afrika timu za Tanzania zimefungwa magoli 3, huku Azam FC wakifungwa goli 3-0 na El-merekh wakati KMKM wakishinda goli 1-0 dhidi Al-hilali.
Yanga SC ndio timu pekee ya Tanzania iliyofanikiwa kusonga mbel kwa jumla ya goli 3-2, huku Azam FC wakitolewa kwa jumla ya magoli 3-2, KMKM kwa jumla ya magoli 2-1 na Polisi kwa jumla ya magoli 8-1.
MATUKIO BILA NAMBA
AZAM WAZUIWA KURIKODI MCHEZO NA KUONYESHA
Katika mchezo wa klabu bingwa Azam TV walizuiwa kuonyesha mchezo kati ya Azam FC na El merekh, ambapo kulivuja taarifa ya kutoruhusiwa kuingia na kamera ya kuchukuwa video katika uwanja wa Merekh pale walipokutana Azam FC na EL-merekh.Lakini kuna video inao eneea mitandaoni inayo onyesha magoli yaliyo fungwa Azam FC, hivyo kuonyesha kuto tendeka kwa agizo hilo kwa vituo vya Sudan.
SIMBA WAKUTANA
Simba SC walikutana jana na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya timu yao, ukiwa ni mkutano wa pili mkuu, wa Simba SC toka uongozi wa Aveva uingie madarakani.TETESI/CHINI YA KAPETI/HAZINA UTHIBITSHO
SIMBA WAMCHEZESHA MCHEZAJI MWENYE KADI TATU ZA NJANO
Taarifa ambayo bado vyanzo vyetu havija thibitisha, inadaiwa kuwa Simba SC wamefanya kosa kumchezesha Ibrahim Ajibu, akidaiwa kuwa na kadi tatu za njano.Kama taarifa hiyo inaukweli ndani yake, huu utakuwa uzembe wa pili kufanywa na klabu hiyo kongwe nchini, baada ya kucheza mchezo wa ligi wakiwa na jezi zisizo na logo ya mdhamini wa ligi.
MWAMAJA KUTOENDELEA KUWA KOCHA WA PRISONS
Wakati Prisons wanacheza na Simba SC juzi, kuna taarifa ya aliyekuwa kocha wa Panoni FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza, yupo katika mazungumzo na uongozi wa Prisons kwa ajili ya kuchukuwa nafasi ya Mwamaja.MATOKEO YA MICHEZO ILIYO TUFIKIA
MATOKEO KLABU BINGWA AFRIKA
EL-MEREKH 3-0 AZAM FCKMKM 1-0 AL-HILALI
MATOKEO KOMBE LA SHIRIKISHO
BDF XI 2-1 YANGAPOLISI 1-3 FC MONANA
MATOKEO LIGI KUU YA VODACOM
SIMBA SC 5-0 TANZANIA PRISONSMGAMBO SHOOTING 0-1 COASTAL UNION
STAND UNITED 2-0 KAGERA SUGAR
MBEYA CITY 1-1 RUVU SHOOTING
MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM
Rn | Timu | P | W | D | L | F | A | Gd | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | YANGA | 15 | 9 | 4 | 2 | 21 | 8 | 13 | 31 |
2 | Azam FC | 15 | 7 | 6 | 2 | 22 | 12 | 10 | 27 |
3 | KAGERA SUGAR | 17 | 6 | 6 | 5 | 13 | 13 | 0 | 24 |
4 | SIMBA SC | 16 | 5 | 8 | 3 | 20 | 12 | 8 | 23 |
5 | Coastal Union | 17 | 5 | 7 | 5 | 11 | 10 | 1 | 22 |
6 | RUVU SHOOTING | 16 | 5 | 6 | 5 | 11 | 12 | -1 | 21 |
7 | STAND UNITED | 17 | 5 | 6 | 6 | 16 | 18 | -2 | 21 |
8 | MTIBWA SUGAR | 15 | 4 | 7 | 4 | 15 | 15 | 0 | 19 |
9 | JKT RUVU | 15 | 5 | 4 | 6 | 14 | 15 | -1 | 19 |
10 | POLISI MORO | 16 | 4 | 7 | 5 | 12 | 14 | -2 | 19 |
11 | NDANDA FC | 16 | 5 | 4 | 7 | 14 | 18 | -4 | 19 |
12 | MBEYA CITY | 16 | 4 | 6 | 6 | 11 | 15 | -4 | 18 |
13 | MGAMBO SHOOTING | 15 | 5 | 2 | 8 | 8 | 16 | -8 | 17 |
14 | T. PRISONS | 16 | 1 | 9 | 6 | 10 | 20 | -10 | 12 |
0 comments:
Post a Comment