Wikend

8 ZASHUHUDIWA MKWAKWANI, IMETOSHA

MATUKIO KATIKA NAMBA

1. GOLI ALILOBAKISHA KAVUMBAGU

Kinara wa magoli msimu huu Didier Kavumbagu amebakiza goli moja kufikisha idadi ya magoli aliyoifungia yanga msimu uliopita, ikiwa ni baada ya jumamosi kufunga goli lake la 9 pale alipoipatia Azam fc ushindi wa goli 1-0 mbele ya JKT Ruvu.

Kavumbagu msimu uliopita alikuwa anaitumikia yanga, ambapo aliifungia magoli 10 katika michezo ya ligi kuu ya vodacom, msimu uliopita ambapo mfungaji bora alikuwa Hamisi Tambwe aliyefunga magoli 19.

2. KADI NYEKUNDU WAKATI MMOJA

Katika mchezo kati ya Azam FC na JKT Ruvu, wachezaji wa wili walionyeshwa kadi nyekundu kwa wakati mmoja, baada ya kufanyiana fujo.

Wachezaji hao ni Salum Aboubakari wa Azam FC na Richard Manyara wa JKT Ruvu, ambao walipewa kadi hizo nyekundu katika dakika ya 59 ya mchezo.

Kadi mbili hizo nyekundi ni nusu ya idadi ya kadi nyekundu zilizotolewa wikiend iliyo pita, ambapo zilitolewa kadi nyekundu 4, ambazo zilikwenda kwa aruna Niyonzima wa Yanga na Othmani wa Coastal union.


2. KADI ZA NJANO WAKATI MMOJA

Katika mchezo wa jana kati ya yanga na simba sc kulishuhudi mwamuzi akitoa kadi mbili za njano wakati mmoja mara mbili.

Mara  ya kwanza ilikuwa ni kwa Ramdhani Kessi na Danny Mrwanda, ambapo ilitokana na Mrwanda kumrejeshea Kessi baada ya kuchezewa faulo na Kessi.

Tukio jingine ni lile kati na Kelvin Yondani na Abdi Banda, baada ya Banda kumgonga Yondani, kada ya njano kwa Yondani nusura isababishe fujo, baada ya wachezaji wa yanga kutaka kumvaa mwamuzi.


4. MAGOLI ALIYEFUNGWA BATHEZ

Goli kipa wa yanga Ally Mustapha Bathez amefungwa goli 4 na Simba SC katika michezo miwili aliypoidakia yanga dhidi ya Simba SC.

Mchezo wa kwanza kuidakia yanga dhidi ya Simba SC Bathez alifungwa goli 3 katika sare ya 3-3, kitendo kilichopelekea kupoteza namba ndani ya yanga kabla ya mwaka huu kurejesha namba yake na jana kuidakia yanga dhidi ya Simba SC na kufungwa goli moja ambalo baadhi ya mashabiki wanaona goli hilo ni la kizembe.


8. MAGOLI YALIYOFUNGWA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI

Katika viwanja ambavyo msimu huu na msimu uliopita haukushuhudia magoli mengi ni uwanja wa Mkwakwani uliopo Tanga, lakini wikiend iliyopita ndio uwanja ulioshuhudia magoli mengi kupita viwanja vingine vyote.

Uwanja wa Mkwakwani umeshuhudia magoli 4 kila mechi iliyochezwa jana na juzi na kupelekea idadi kuwa ya magoli 8 kufungwa.

Uwanja wa Manungu ulishuhudia magoli mawili huku uwanja wa Taifa na Azam Complex ukishuhudia goli 1 kwa kila uwanja.

Mechi ya kwanza kushuhudia magoli manne ulikuwa ni mchezo kati ya Coastal union na Kagera sugar uliomalizika kwa sare ya goli 2-2 na kisha kushuhudia Mgambo wakiwalaza Ndanda FC kwa magoli 3-1.


52.GOLI LA OKWI

Emanuel Okwi alifunga goli katika dakika ya 52 ambayo ukigeuza namba za dakika kwa kutanguliza namba ya mwisho na ya kwanza kuwa ya mwisho unapata namba ya jezi anayo penda kuivaa ambayo ni 25.

MATUKIO NNJE YA NAMBA

IMETOSHA MAUAJI

Katika mchezo wa jana kati ya Simba SC na Yanga ulisindikizwa na ujumbe wa 'IMETOSHA UWAJI WA ALBINO'.
Mpira wa miguu kwa muda mrefu umekuwa ukitumika kufikisha ujumbe kwa jamii, na muda mwingine kusimamisha vita katika maeneo tofauti.

TFF walitumima fursa ya mchezo wa simba na yanga kuonwa na watu wengi, kufikisha ujumbe juu ya tatizo yanayo wakumba ndugu zetu Malbino, ambao wameripotiwa kupoteza maisha kikatili na kunyofolewa viungo vya kikatili kwa imani potofu za kishirikina.
 

TAULO LA IVO

Kabla ya matanage kuanza kati ya Simba na yanga, Ivo mapunda alizozana na mwamuzi wa mchezo juu ya mahali pakuliweka taulo lake, wakti Ivo akitaka kulininginiza kwenye nyavu, wakati mwamuzi akimuamuru aliweke kando ya goli.

Ivo alitii amri baada ya kuzozana kwa dakika moja, na alilitandika taulo lake nyuma pembeni mwa goli.

Baada ya goli la Emanuel Okwi taulo la Mapunda liliamishiwa kwenye bango la vodacom lililokuwa nyuma ya goli la Mapunda.


VIRUSI YANGA

Ni jambo la kwaida kwa wachezaji kushtumiwa katika soka la bongo mara baaday a michezo mikubwa kumalizika , ambapo mashabiki wa yanga, jana walilalama kuwa katika kikosi chao kuna virusi, ambavyo vimepelekea wao kufungwa goli 1-0 mbele ya Simba SC.

Mashabiki hao wa yanga kwa nyakati tofauti wamesikika wakitaka viongozi kutoa virusi vilivyomo ndani ya yanga.


MSEMO WA WIKI TOKA KWA JB

Mtengeza filamu na muigiza mashuhuri nnchini JB jana katika makala ya Simba na yanga iloyo onyeshwa na Azam TV, alisema kuwa 'ATA BARCELONA WAKIBADILISHWA JINA NA KUWA YANGA, WAKIKUTANA NA SIMBA SC, LAZIMA SIMBA WASHINDE'.

MATOKEO YALIYOTUFIKIA

LIGI KUU TANZANIA BARA

JKT RUVU 0-1 AZAM FC
SIMBA SC 1-0 YANGA SC
MTIBWA SUGAR 1-1 MBEYA CITY
COASTAL UNION 2-2 KAGERA SUGAR
MGAMBO SHOOTING 3-1 NDANDA FC

MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARAA

RnTimuPWDLFAGdPts
1YANGA169432191231
2Azam FC1686223121130
3SIMBA SC176832112926
4KAGERA SUGAR186751515025
5MTIBWA SUGAR175841817123
6Coastal Union185851312123
7NDANDA FC186481722-522
8STAND UNITED175661618-221
9RUVU SHOOTING175661214-221
10JKT RUVU175571416-220
11MGAMBO SHOOTING166281117-620
12POLISI MORO174761316-319
13MBEYA CITY174761216-419
14T. PRISONS1711061020-1013

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.