mingine

MBIO ZA MBUZI MEI 30

MASHINDANO ya 15 ya mbio za hisani za Mbuzi yanatarajiwa kufanyika Dar es Salaam Mei 30, mwaka huu.

Mwenyekiti wa mashindano hayo Karen Stanley alisema jana kuwa mbio hizo zinatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya The Green, barabara ya Kenyatta, ambapo zimelenga kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia vituo vinavyojihusisha na makundi maalumu.

Alisema tangu mashindano hayo yaanze kufanyika mwaka 2001, mbio hizo zimechangisha zaidi ya Sh milioni 980 kwa ajili ya vituo vya hisani, na mwaka huu wanatarajia kuweka rekodi ya Sh bilioni moja.

“Kila mwaka tumeweza kufanya tukio hili kutokana na msaada tunaopata kutoka kwa wafadhili na bila kusahau watu wanaojitokeza siku ya mashindano kila mwaka,” alisema.

Alisema wakati siku ya kufanyika tukio hilo ikitangazwa, watu na taasisi mbalimbali wanahamasishwa kujitokeza na kumiliki mbuzi huku akiongeza kuwa kumiliki mnyama huyo ni jambo lenye bashasha nyingi, hasa inapotokea akishinda na wakati huo ikisaidia kuchangisha fedha.

Alisema Mbuzi hao ni wachache hivyo wanaotaka kumiliki wanatakiwa kuwasiliana nao kwa njia ya barua pepe.

“Kwa wale wanaotaka kushiriki katika mashindano ya mavazi, kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Bollywood’ kiwanda cha filamu nchini India inayoweza kuleta msisimko wa pekee,” alisema na kuviomba vituo vya hisani vilivyosajiliwa kutembelea tovuti yao na kujaza fomu kwa ajili ya msaada.

Alisema mbio hizo zingekuwa hadithi kama si msaada wa wafadhili na kushukuru waliowaunga mkono mwaka huu ikiwa ni pamoja na Hoteli ya Southern Sun, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), benki ya CBA, Coca-Cola, Toyota, Tigo, Regent Tanzania, Shirika la Ndege la Uswisi na Continental Outdoor.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.