netball

NIC HAIKAMATIKI AFRIKA MASHARIKI

Na Mwajuma Juma, Zanzibar

TIMU ya netiboli ya NIC ya Uganda imeendelea kutesa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki baada ya jana kuwafunga ndugu zao wa Prisons mabao 35-32 kwenye uwanja wa Gymkhana mjini hapa.

NIC ambayo inaongoza katika kundi A ikiwa na pointi 8, haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa michuano hiyo ambayo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii.

Prisons ya Uganda inaminyana kwenye nafasi ya pili na Uhamiaji zote zikiwa na idadi ya pointi sita kila moja wakitofautiana kwa idadi ya magoli.

Katika kundi B, timu ambayo inaongoza ni MOICT ya Kenya ikifuatiwa na KCCA ya Uganda yenye pointi 4 ambayo imebakiwa na mchezo mmoja wakati Mafunzo inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi mbili na kubakisha michezo miwili.

Michezo mingine iliyochezwa jana katika uwanja huo ni ule uliowakutanisha Uhamiaji ambayo ilishinda mabao 52-38 dhidi ya timu ya Zimamoto ambayo inashika mkia katika kundi hilo A.

Aidha, mchezo mwingine uliochezwa mapema jana ulikuwa ni kati ya KCCA ya Uganda na KVZ ambao ulimalizika kwa KCCA kushinda mabao 40-28.

KVZ ambayo ni mara yake ya kwanza kushiriki michuano hiyo imepangwa katika kundi B, na inashika mkia katika kundi hilo.

Chanzo: HABARI LEO

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.