vilabu

POLISI DODOMA YAUZWA

TIMU ya soka ya Polisi Dodoma imeuzwa kwa wadau wa soka katika Wilaya ya Mpwapwa kwa lengo la kuhakikisha Mkoa wa Dodoma unapata timu itakayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara misimu ijayo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano kati ya wadau wa soka wilayani Mpwapwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime, kamanda huyo alisema wameamua kuwapa timu hiyo wakazi wa Mpwapwa kutokana na kuwa na nia ya dhati ya kuhakikisha Mkoa wa Dodoma unapata timu itakayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Polisi Dodoma ilimaliza ligi hiyo katika nafasi ya 11 kati ya timu 12 za Kundi B kwa kujikusanyia pointi 19.

Mwadui FC ya Shinyanga na Toto Africans ya Mwanza zilipanda kutoka kundi hilo zikiungana na African Sports ya Tanga na Majimaji ya Songea kucheza Ligi Kuu msimu ujao wa 2015/16. Kamanda Misime alisema ni muhimu kwa timu hiyo ikaanza maandalizi mapema.

Akizungumzia suala la timu hiyo kubadili jina, Kamanda Misime alisema jambo hilo lipo katika mchakato na watakutana wiki ijayo kujadiliana ni jina gani watatumia ili kushiriki Ligi Daraja la Kwanza katika msimu unaokuja.

Msemaji wa wadau wa mkoani Mpwapwa waliokuja kukabidhiwa timu hiyo, Rashid Msangi alilishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwapatia timu hiyo.

CHANZO: HABARI LEO

About kj

1 comments:

Unknown said...

Haya sasa wana mpwapwa...kinachotakiwa ni kujitoa kwa wingi ili kuipa support timu yetu ili turudishe burudani ambayo tuliipoteza na kuimiss kwa muda mrefu...kwa pamoja tunaweza...mbele daima nyuma mwiko.

Powered by Blogger.