
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Tava, Agustino Agapa alisema mafunzo hayo yatafanyika kwa wiki nzima na kuendeshwa na mkufunzi wa kimataifa kutoka Ujerumani.
Agapa alisema mafunzo hayo pia yatawahusu walimu wa michezo wa vyuo na klabu mbalimbali na kwamba yamepangwa kufanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
“Mafunzo haya ni utaratibu wetu katika kuhakikisha tunawapa elimu wadau wetu ili wakawe mabalozi wazuri katika sehemu zao za kazi,” alisema.
Alisema baada ya mafunzo hayo wanategemea wataibua vipaji vingi kwa ajili ya kuunda klabu ambazo zitakuwa zikishiriki michuano kwa ushindani mkubwa ndani na nje ya nchi.
CHANZO: HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment