Michezo hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa Gymkhana kwa nyakati tofauti ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa ni kati ya Uhamiaji na JKU ambao ulimalizika kwa Uhamiaji kushinda mabao mabao 37-31.
Katika mchezo huo ambao ulichezwa saa 2:30 za asubuhi ulionesha ushindani mkubwa ulioleta faraja kubwa kwa mashabiki waliohudhuria uwanjani hapo.
Uhamiaji ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja katika mchezo huo mabao yake yalifungwa na Kiache Sharo (22) na magoli 15 yakifungwa na Jawa, wakati kwa upande wa JKU ambayo ni mechi yake ya pili kupoteza mabao yake yalifungwa na Pili Peter na Dawa Haji.
Kwa upande wa timu Prisons ilishuka uwanjani saa 3:45, iliondoka na ushindi wa mabao 59-33 dhidi ya Zimamoto. Katika mchezo huo, Prisons ili watumia wafungaji wake Stela Atai na Florence Amono wakati wafungaji wa Zimamoto ni Asha Ibrahim na Asma Khamis.
Aidha katika mechi nyingine, mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya NIC iliifunga JKT Ruvu mabao 38-16, huku mabao yake yakifungwa na Stela Oyera na Hadijah Nakabuye.
Nayo Mafunzo na KCCA ya Uganda ziliumana na timu ya KCCA kushinda kwa ushindi mwembamba wa mabao 37-36.
CHANZO: HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment