LEO MEI MOSI
Hivi sasa katika viwanja vya leaders club kuna bonanza la mchezo wa soka unahusisha makampuni mbali mbali yanayoshirikiana na kipindi cha Sports Xtra cha Clouds FM.
Mashindano hayo yatachukuwa siku nzima ya leo, ambapo timu nane zinashiriki sambamba na timu yaclouds FM, katika hilo bonanza lililo andaliwa na Sports Xtra ikiwa ni sehemuyakukutana na wadau wa kipindi hicho.
KESHO MEI PILI
ETOIL DUSAHEIL Vs YANGA
Katika ardhi ya Tunisia kesho timu ya Tanzania itakuwa ina tupa karata yake ya kusaka nafasi ya kuingia katika 16 bora ya kombe la shirikisho, endapo watapata ushindi au sare ya kuanzia goli 2-2.
Yanga SC (Wakimataifa) ndio wahusika wa mechi hiyo baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa bara mwanzoni mwa wiki hii.
Mchezo ho ambao utaanza katika majira ya saa moja usiku kwa masaa ya Tunisia ikiwa ni sawa na saa tatu kwa saa za Tanzania, mpaka sasa hakuna kituo cha television kilichotangaza kuonesha mchezo huo zaidi ya kituo cha EFM kutangaza kuutangaza mchezo huo, na ukurasa wako waSIB Dakika 90 utakuletea matokeo ya moja kwa moja toka Tunisia.
Katika mchezo huo wa kesho yanga inaongezwa nguvu na urejeo wa Salum Telela na Adrey Countinho walioukosa mchezo wa awali, huku na urejeo wa nahodha wao Nadir Haroub ailiyeshindwa kuumaliza mhezo wa kwanza uliochezwa katika uwanja wa Taifa.
MBEYA DARBI
Katika jiji la Mbeya siku ya ya lesho kutakuwa na mchezo wawapinzani wa Mbeya kati ya Mbeya city na Tanzania Prisons, mchezo utakao chezwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Prisons wanahitaji ushindi ilikujiweka katika maingira mazuri ya kutoshuka daraj, wakati Mbeya city watakuwa hawanacha kupoteza zaidi ya kusaka ushindi ili wamalize mahala pazurikatika msimamo wa ligi.
Kesho itakuwa darb ya nne kukutana katika ligi kuu ya vodacom toka Mbeya city iande ligi kuu msimu uliopita.
MICHEZO MINGINE YA KESHO
NDANDA FC Vs KAGERA SUGAR, uwanja wa Nangwanda Sijaona
MGAMBO SHOOTING Vs JKT RUVU, uwanja wa CCM Mkwakwani
KESHO KUTWA MEI 3
WINDO LA KUIWAKILISHA TANZANIA
Siku yajumapili katika uwanja wa Taifa kutakuwa na mtanange wa kusaka nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa, pale Azam FC watakapo wakabili Simba SC katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya vodacom.
Ushindi wa Azam FC katika mchezo huo una maansha kukosekana kwa Simba SC katia mwaka watatu mfululiozo katika michuano ya kimataifa kutokana na Azam FC kufikisha pointi 48 ambazo hawawezi kuzifikia.
Ushindi wa Simba SC kutapelekea hatma ya o kuangukia kwa yanga siku ya jumatano, pale yange watakapo wakabili Azam FC, kwani baada ya mchezo huo kutakuwa natofauti ya pointi moja.
Na mchezo huo uimalizika kwa sare Azam waatkuwa teyari wamejiahhakikshia kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa mwakani katika kombe la shirikisho ikiwa ni mara ya 4 mfululizo.
Mara ya mwisho kukutana mchezo ulimalizika kwasare mchezo uliochezwa mapema mwaka huu.
MICHEZO MINGINE YA MEI 3
COASTAL UNION Vs STAND UNITED MkwakwaniMTIBWA SUGAR Vs RUVU SHOOTING Manungu
0 comments:
Post a Comment