mingine

FAINALI MBIO ZA BEISKELI JUMAMOSI

FAINALI za mashindano ya mbio za baiskeli Kanda ya Ziwa zinatarajiwa kufanyika Jumamosi ya wiki hii mkoani ya Shinyanga na kushirikisha washiriki wanawake na wanaume wapatao 250.

Akizungumza na gazeti hili jana, Rais wa Chabata Geofrey Mhagama alisema mashindano hayo yanayofahamika kama Acacia Kanda ya Ziwa baiskeli yanatarajiwa kupata wachezaji bora 30 watakaoingia kwenye mashindano ya Taifa yatakayofanyika baadaye mwaka huu.

Alisema jumla ya mikoa sita itashiriki mbio hizo ambayo ni Shinyanga, Geita, Kagera, Simiyu, Mwanza na Mara.

“Tupo huku tukiendelea na maandalizi kuhakikisha tunakamilisha michuano hii ya Acacia kwa lengo la kupata wachezaji bora watakaoingia kwenye ushindani wa taifa, tunategemea kutakuwa na upinzani mkali,” alisema.

Alisema mshindi wa kwanza atajinyakulia Sh milioni moja na nusu kwa wanaume wakati wanawake wataondoka na Sh milioni moja na laki mbili.

Aidha, alisema washindi 30 kwa wanaume watapata kila mmoja Sh laki moja na nusu na wengine 20 kwa wanawake wataondoka pia na kiwango hicho.

Mhagama alisema mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ambapo hutafuta wachezaji bora wa kanda hiyo kuwakilisha katika mashindano ya kitaifa.

Alisema mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Juni 25-26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.


chanzo: habari leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.