tenesi

TANZANIA YAFANYA VIBAYA TENESI AFRIKA

TANZANIA imeshindwa kung’ara katika michuano ya tenisi ya Acacia Afrika baada ya kutolewa katika hatua ya nusu fainali jana na wageni.

Wachezaji pekee waliobaki katika hatua ya nusu fainali kwa hatua ya mchezaji mmoja walikuwa ni wawili kati ya 34 walioshiriki awali, na hivyo kuwaachia nafasi nchi za Kenya, Uganda na Zambia.

Watanzania walioshindwa kwenye hatua ya nusu fainali ni Rehema Athuman ambaye alikubali kichapo cha seti 6-0, 6-2 kutoka kwa mchezaji wa Kenya Otula Evelyn.

Aidha, mchezaji mwingine ambaye aliishia kwenye hatua hiyo ni Omar Abdallah baada ya kukubali kichapo kutoka kwa Mzambia Kazembe Edger cha seti 6-3, 6-3 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Gymkhana.

Wachezaji Shufaa Changawa wa Kenya alitinga fainali baada ya kumshinda mwenzake Paige Mbugua kwa seti 6-0, 6-1 na Oring David wa Uganda alimshinda Mkenya Khan Fazal kwa seti 6-3, 6-3.

Chanzo: habari leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.