mingine

Wigo mashindano ya Ngalawa wapanuliwa

KAMPUNI ya COMNET ambao ni wadhamini wa mashindano ya mbio za Ngalawa, wameamua kupanua wigo wa mashindano hayo ambapo kwa mwaka huu yatafanyika Bagamoyo na Dar es Salaam kabla ya kufanyika Zanzibar wakati wa Tamasha la ZIFF.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Mashindano hayo Omary Mdogwa alisema tamasha la ZIFF ni tamasha la utamaduni na nembo yake ni Jahazi, hivyo mbio hizo za ngalawa zimeshikiliwa na ZIFF kama njia mojawapo ya kuendeleza utamaduni wa Zanzibar na wa nchi za Jahazi.

“Kila mwaka wakati wa ZIFF tunakuwa na mashindano ya Ngalawa, kwa mwaka huu tumeamua kupanua wigo na hivyo yatafanyika Bagamoyo kesho (leo) kwenye ufukwe wa Millenium Hotel na kwa Dar es Salaam yatafanyika kwenye ufukwe wa Msasani,” alisema.

Mdogwa alisema washindi wa kwanza kutoka Bagamoyo na Dar es Salaam watapelekwa Zanzibar kushindana na majahazi mengine 10.

Alisema mbio za mwaka huu za ZIFF zitakuwa za kipekee kwa kuwa zitafanyika siku ya Eid pili Julai 19 na zinatarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 20,000 katika ufukwe wa bahari wa Forodhani kushuhudia mbio hizo.


CHANZO HABARI LEO

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.