
Maombi ya vitambulisho vya waandishi wa habari kwa ajili ya michuano ya CECAFA Kagame Cup 2015 yamefunguliwa rasmi kuanzia leo tarehe 7 Julai, 2015 katika tovuti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF.
Kila Kampuni ya Habari (Media House) inaombwa kuomba vitambulisho vitano (5) vya waandishi wa habari watakaofanya kazi wakati wa michuano ya kombe la Kagame Cup kwenye tovuti ya TFF (tff.or.tz) kisha kuchagua KAGAME CUP, ACCREDITATION na kujaza fomu ya maombi ya kitambulisho na kuambatanisha na picha ya muombaji.
Mwisho wa kuomba kitambulisho kwa waandishi wa habari ni jumatano tarehe 15 Julai, 2015 saa 6 kamili usiku.
Waombaji wa vitambulisho hivyo wote wanaombwa kufanya maombi hayo mapema ili kuondokana na usumbufu wakati michuano ya Kagame itakapokua imeanza.
Fuata link hii kujaza maombi ya kitambulisho http://tff.or.tz/kagame-cup-2015/accreditation
0 comments:
Post a Comment