MINZIRO: NIDHAMU KWANZA
KOCHA Mkuu wa timu ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, Fred Felix Minziro amewataka wachezaji wa timu hiyo kuwa na nidhamu ya mchezo iwe mazoezini au katika mechi.
Aliwasisitiza wachezaji hao kuwahi katika eneo wanalohitajika kwa muda uliopangwa ili kwenda sambamba na programu za kocha.
“Kazi ya mpira ni ngumu inahitaji mchezaji ajitume kadri ya uwezo wake na awe na uzalendo wa jukumu lililo mbele yake,” alisisitiza kocha huyo.
“Sitokuwa na masihara na mchezaji yeyote ambaye hatajituma. Ligi imeanza hivyo kuanzia sasa mjione mpo kazini kilichopo ni kuangalia ratiba na programu za mazoezi.”
Kocha huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na wachezaji wa timu hiyo kwenye uwanja wa mazoezi Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa uliopo Mlalakuwa jijini Dar es Salaam juzi.
Kwa upande wa mchezo wao na timu ya Mbeya City utakachezwa mkoani Mbeya, Minziro aliwataka wachezaji hao kujiandaa vizuri kwa mpambano huo. Kwa upande wa timu, kocha huyo alisema timu ipo vizuri.
0 comments:
Post a Comment