CECAFA

GOR MAHIA WATIBUA SHEREHE YA EID JANGWANI, CANNAVARO AKIKOSA PENATI, NGOMA APIGWA UMEME

Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC leo wamekubali kichapo cha goli 2-1 toka kwa Gormahia katika mchezo wa kombe la Kagame uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa leo Yanga walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Donald Ngoma katika dakika ya 4 ya mchezo kabla ya Gormahia kusawazisha katika dakika ya 16 kupitaia kwa Haruna Shakava.

Katika dakika ya 24 Donald Ngoma alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kumrushia ngumi Haruna Shakavu ikiwa ni kadi yake ya pili ya njano na kupelekea yanga kumalizia dakika wakiwa pungufu.

Kutolewa kwa Ngoma kwa kadi nyekundu kuliwapa utawala mchezo Gor mahia, huku yanga muda mwingi wakitumia kuokoa hatari za Gor mahia, na kushuhdia timu zikienda mapumziko zikiwa sare ya goli 1-1.

Gor mahia walirejea kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kuandika goli la pili  kupitia kwa Michael Olunga katika dakika ya 47, goli hilo liliwatuliza zaidi Gor mahia huku yanga wakihangaika kusaka nafasi ya kupata goli la kusawazisha.

Yanga katika dakika ya 72 walipata penati kufuatia beki wa Gor mahia kuushika mpira ndani ya 18 na penati hiyo iliyopigwa na Nadir Haroub Cannavaro iliokolewa kifasaha na kipa wa Gormahia.

Kukosa kwa penati hiyo kuliiamsha yanga sc na kuendelea kusaka goli bila mafanikio, na mchezo kumalizika kwa Gor mahia kuibuka na ushindi wa goli 2-1.


About kj

1 comments:

Jomki said...

Yanga were the better team even with 10 men they gave a good fight..

Powered by Blogger.