mingine

OLIMPIKI MAALUM WAPATA MAADILI

Frank Macha
WANARIADHA watatu wa mbio za mita 400 wa timu ya Olimpiki Maalum inayoshiriki mashindano ya dunia yanayofanyika Marekani wamepata medali.

Akizungumza kwa njia ya mtandao kutoka Los Angels, Marekani jana, Mkuu wa msafara, Frank Macha alisema Tanzania iliingia katika hatua ya fainali kwa mchezo wa riadha na kufanikiwa kutwaa medali.

“Wachezaji wetu wamefanikiwa kupata medali tatu ambazo Godfrey Jabuya alikuwa wa kwanza na kupata medali ya dhahabu, Blandina Patrick akashika nafasi ya pili na kujinyakulia medali ya fedha na Deonatus Manyama akaambulia Medali ya Shaba baada ya kushika nafasi ya tatu,” alisema Macha.

Pia alisema wachezaji wengine wawili walioingia fainali hawakufanya vizuri sana japokuwa walishika nafasi ya sita na ya nane. Alimtaja Riziki Chilumba kuwa alishika nafasi ya sita kwenye mita 400 na David Kenyamaho alishika nafasi ya nane kwenye mbio za mita 200.

“Fainali nyingine zitaendelea kesho na kwa bahati mbaya ninapotuma taarifa hii ratiba ilikuwa haijatoka. Uwezekano wa kupata medali zaidi ni mkubwa kwa hiyo kila siku nitawapa taarifa,” alisema.

Timu hiyo ina wachezaji wanane, wanawake wanne na wanaume wanne, itashiriki katika mchezo wa riadha katika mita 100, 200, 400, 800, 5000, nusu marathon na mita 4x100 kupokezana vijiti. (Relay).

CHANZO: HABARI LEO

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.