Lakini historia ya kuvutia zaidi ni kutwaa ubingwa wa kimataifa wa CECAFA Kagame Cup kwa kucheza mechi sita za mashindano na timu mabingwa bila kupoteza mchezo hata mmoja.
Uongozi wa Azam FC umethibitisha kwa vitendo kuwa haukukosea kumrejesha Kocha Muingereza Stewart Hall klabuni baada ya kukaa nje ya klabu kwa miezi 13 kwani miezi miwili tuu baada ya kutua amewezesha klabu kutwaa kikombe kikubwa baada ya kuwachapa Gor Mahia ya Kenya bao 2-0.
Katika mchezo huo, Azam FC ilicheza soka la mbinu za ushindi ikitumia fomesheni ya 3-5-2 waliipoteza kabisa Gor Mahia hasa washambiliaji wake Meddy Kagare na Michal Olunga ambao hawakufulukuta kwa ngome iliyoongozwa na Serge Wawa Pascal.
Azam FC ilifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa, Ame Ally na kumwingiza Frank Domayo dakika 46 Farid Mussa akaingia Erasto Nyonni na Tcxhetche alitoka akaingia Didier Kavumbagu dakika ya 86
Azam FC pia imeweka historia ya aina yake baada ya wachezaji wake kushinda tuzi za mchezaji bora kila mechi. beki wa kati, Muivory Coast, Serge Wawa 'Waziri wa Ulinzi' amekuwa mchezaji bora wa mechi tatu huku Salum Abubakar, Farid Mussa Shah na Aishi Salum Manula wakishinda tuzo hiyo mara moja kila mmoja. Kwa maana hiyo wachezaji wa Azam FC walishinda tuzo za mchezaji bora wa mechi kwenye kila mchezo.
Kivutio kingine ni kwa Serge Wawa Pascal kuwa mchezaji bora wa mashindano huku mlinda lango Aishi Manula akishinda tuzo ya nyanda bora wa mashindano.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Said Morrad,Aggrey Morris, Serge Wawa, Mugiraneza Jean Baptiste, Himid Mao, Kipre Tchetche/Kavumbagu, Ame Ally/Frank Domayo, Bocco, Farid Mussa/ Erasto Nyoni.
0 comments:
Post a Comment