Wikend

AZAM WASHINDA, MTIBWA WACHAPWA, YANGA NA MBEYA CITY KESHO KUJIANDAA NA VPL

Mfungaji wa goli la kwanza la Simba SC hii leo dhidi ya URA ya Uganda, Kelvin Ndayisenga
Leo michezo mitatu ya kirafiki ya timu zinazo jianda na ligi kuu ya vodacom imechezwa katika viwanja vitatu tofauti huku kesho kukitarajiwa kuchezwa michezo miwili.

Wakati Simba SC wakiibuka na ushindi wa goli 2-1 katika uwanja wa taifa dhidi ya URA ya Uganda, Mtibwa sugar wao wamerkubali kichapo cha goli moja mbele ya Ruvu shooting ya Pwani mchezo uliochezwa katika uwanja wa Mabatini.

Katika mchezo huo wa kirafiki Ruvu shooting walipata goli lao pekee kupitia kwa Yahya Tumbo, na kuipa ushindi wa goli 1 timu hiyo iliyo shuka daraja msimu uliopita mbele ya wakatamiwa wa Manungu, Mtibwa Sugar.

Katika mchezo mwingine wa kirafiki uliochezwa usiku huu Azam FC wamibuka na ushindi wa goli 3-0 mbele ya Mafunzo, magoli ya Azam FC yakifungwa na Shomari Kapombe katika dakika ya 37, Aggrey Morice kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 50 na John Bocco akimalizia pasi ya Ramadhan Singano katika dakika ya 71.

Kesho katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam Mwadui FC ya Shinyanga itacheza dhidi ya Frands Rangers inayoshirriki ligi daraja la kwanza, huku mkoa ni Mbeya Yanga SC wakipimana ubavu na Mbeya city katika uwanja wa Sokoine.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.