Kocha mpya wa African Lyon, Edwardo Filipe Almeida (kushoto) wakati alipokuwa akitambulishwa na Mmiliki wa timu hiyo, Mohamed Dewji (Hii picha ni ya mwaka 2009). |
17.03.2009.. Mo. Dewji aliinunua timu iliyopanda ligi kuu, ilikua ikiitwa Mbagala Market. Mda mfupi baada ya ununuzi huo, aliibadili jina na kuiita African Lyon.. Timu hii alidumu nayo kwa mda wa mwaka mmoja tu.. mambo yakawa magumu upande wake.. akaona isiwe tabu.. akaipiga bei kwa Ndg. Rahmu Kagenzi "Zamunda".
Miaka 5 baadae.. Mo. Dewji anaibuka na ndoto yake ile ile ya kutaka kumiliki timu inayoshiriki ligi kuu. Hapa anataka kujaribu bahati yake Simba S.C.. kwa kuomba apewe 51% ya umiliki wa Timu.. Huku yeye akiwekeza 20 bilioni katika Timu.
Simba S.C ni "taasisi" kubwa yenye fanbase kubwa pia.. Hivyo kuiongoza inahitaji uwe na "Moyo Mkubwa".. Je ule "Moyo Mdogo" uliokufanya ubwage manyanga African Lyon, sasa hivi umeshakua Mkubwa?
Je hivi sasa neno "hasara" halipo katika misamiati yako?.. Maana hofu yangu kuu ni kua mambo yakienda kombo katika timu yetu pendwa unaweza ukatutelekeza njiani.. huku ukielekeza lawama lukuki kwa wamiliki wengine [49%].. kua wanakwamisha mipango yako.
Kipindi Mo. Dewji anakabidhiwa Mbagala Market.. alikuja na ahadi hii.. ".. tayari nimeshanunua kiwanja ambacho nategemea kujenga kiwanja cha kisasa cha soka kitakachokuwa na viwanja vya michezo mingine kama vile sehemu ya gym ,maduka na hosteli za kulala wachezaji"
Ndg. Mo Dewji miaka mitano baada ya ununuzi wa hicho kiwanja, maendeleo ya ujenzi yakoje?
USHAURI WANGU KWA Mo. Dewji.
1. Ndg. Mo. Dewji kama una nia ya dhati ya kuokoa soka letu, si lazima uje Simba S.C.. fuata nyayo za mabilionea wengine.. kwa kununua timu iliyo Ligi daraja la kwanza.. Hapo utakua huru kuimplement kila unachotaka kukifanya.
2. Kama ndoto yako ni kuifanya Simba S.C iwe ya Ki Ulaya Ulaya zaidi.. Si lazima uwe mmiliki.. Kuna bodi ya wadhamini, nadhani huko kuna "kiti" chako.
USHAURI WANGU KWA uongozi wa Simba S.C.
Kipindi tunaendelea kuipitia hiyo "paper" aliyoileta.
1. Naomba mkumbuke kumuuliza maswali hayo hapo juu.
2. Pia "Muwe makini.. Musije mkabidhi Mbu kazi ya kutibu Malaria"
PERUZI ZA MSUNI ZIKAKUTANA HII TOKA MTAA WA www.mohammeddewji.com
I am a huge fan of the local football league and sports in Tanzania especially footie.Recently I bought The Mbagala Market football club which is now known as African Lyon Football Club .It was in the first division and this season it got promoted to Premiership division for the 2009-10 season. African Lyon for me is not just a team but a great project for Tanzania which would help to promote the local footballers all over the world.
My aim is to enable Africa Lyon to play in its very own stadium which will help the team gain its own revenues independently. I want to see African Lyon in the league of continental tournaments against the likes of Al Ahly and Asec Mimosas.
Players like Yaya Toure and Kolo Toure were competing with Asec Mimosas of Ivory Coast and now they have moved to the next level in the Champions League of Europe. I want to make sure Tanzanians hold their head in pride like the people of Ivory Coast one day in seeing win at the highest levels.
I would like to welcome all those stakeholders and fans of Tanzanian soccer to support this Project of African Lyon FC .
As the owner of a football club I haven't forgotten my original responsibility towards our national team Taifa Stars and I believe the presence of African Lyon in Tanzania gives both teams a healthy opportunity to compete and ultimately participate and win the African Nations Cup and the World Cup in future.
mwisho wa nukuu
0 comments:
Post a Comment