mtazamo

TUSIPOKUWA MAKINI TUTAENDELEA KUWA MASHUHUDA KWA KAMATI ZETU

Na Abood Msuni

Mwaka 2004 timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boy) ilifanikiwa kufuzu kucheza mataifa ya Afrika kwa matokeo ya uwanjani kabla ya kashfa ya umri wa mchezaji Nurdin Bakari, kupelekea kuondolewa katika mashindano hayo.

Na kumbuka mwaka huo aliyekuwa kocha msaidizi marehemu Marsh alikuwa akionekana kwenye kituo cha luninga cha ITV akiomba wadau waisaidie timu hiyo kwa hali na mali.

Sina kumbukumbu ya kuwepo kwa kamati ya saidia timu hiyo ya viajana ili iweze kufuzu ambapo walifanikiwa kufuzu jambo walizuiwa kushiriki kutokana na udangajifu wa umri.

Kipindi cha kocha Marcio Maximo iliundwa kamati ya Saidia Stars, ambayo ilisaidia kuamsha uzalendo kwa kuipenda na kuitambua timu yetu ya Taifa, na siku walipocheza na Msumbiji kwa mara ya kwanza katika dimba la la Taifa kila mtu alitambua Taifa stars siku hiyo inacheza, hususani wale wa kazi wa jiji la Dar es salaam ambapo mchezo huo ulichezwa..

Kamati hiyo kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kuamsha hamasa za mashabiki wa soka nchini, japo kuwa hatukufanikiwa kufuzu kombe la mataifa ya Africa mwaka 2008 lakini walifanikiwa kufuzu mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani mwaka 2009 yaliyofanyika nchini Ivory coast.

Baada ya michuano hiyo hatukubahatika kuiona stars bora katika kipindi alichomalizia kocha Marcio Maximo kabla ya kutimka nchini mwezi wa 6 mwaka 2010.

Na katika kipindi hicho cha matokeo mabovu ya stars chini ya Marcio Maximo sikupata kusikia kamati yoyote ile japo kulikuwa hakuna taarifu ya kuvunjwa kwa kamati ya Saidia Stars ishinde.

Kipindi cha kocha Kim Poulsein aliundiwa kamati ambayo malengo yake ilikuwa ni kufuzu kombe la dunia lililofanyika nchini Brazil mwaka jana ambapo Stars ilipoteza mwelekeo baada ya kuudniwa hiyo kamati.

Wiki za hivi karibuni stars ya Mkwasa nayo imeundiwa kamati ya kuhakikisha inafanya vyema katika mchezo ujao wa kusaka tiketi ya kfuzu kombe la dunia dhidi ya Algeria.

Kama kamati hiyo itakuwa na malengo nnje ya kupata matokeo mbele ya Al-geria, itakuwa na faida, ila ni kama ya kupata matokeo katika mchezo huo, basi haitokuwa na tofauti na kamti zilizopita ambazo kwangu ni kama kamati za harusi.

Hakuna Mtanzania ambaye hataki Taifa stars ipate matokeo mbele ya Al-geria hapo katikati ya mwezi ujao, ila tunakuwa na mwendelezo gani baada ya hapo, ama kila hatua ya kufuzu tuna anza moja?

Nina uhakika kama kamati ya Saidia Stars ya kipindi cha Marcio Maximo ingekuwa haija angalia malengo ya karibu ambayo ilikuwa ni kufuzu AFCON 2008, basi nina imani kusingekuwa na haja katika kuelekea kuikabili Al-geria mechi za november 7 na 8 za ligi kuu ya vodacom kusogezwa mbele, kwa kuwa wachezaji wetu wangekuwa bora maradufu ya ubora waliokuwa nao.

Nina imani mashabiki kuelekea mchezo huo wote wangekuwa na imani ya timu yao kushinda katika mchezo huo.

Kamati za harusi hazito tufikisha popote pale katika medali za kimataifa kama tutaendele kuzifanya zionekane za harusi badal ya kuonekana kama za maafali ya vyuo, ambapo kila mahafali moja inapokwisha huanza maandalizi ya mahafali inayokuja kwa kuziba mapungufu yaliyojitokeza katika mahafali yaliyo pita.

Na tuache utamaduni wa kuunda kamati katikati ya mashindano kama kweli tunaamini kamati inaweza kutosogeza pale tunapotaka kwenda.


About kj

0 comments:

Powered by Blogger.