CECAFA

STARS WAPANGIWA NA ETHIOPIA NA ZAMBIA CHALENGE


Makundi ya kombe la la mataifa ya Afrika Mashariki na Kati 'Chalenji Cup' yametangazwa huku Tanzania Bara "Kilimanjaro  Stars" wakipangwa katika kundi A pamoja na wenyeji Ethiopia.

Michuano hiyo inayo taraji kuanza november 21 nchini Ethiopia yatafanyika katika majiji matatu nchini humo, wakati timu shiriki zimegawanywa katika makundi 3.

Wakati Kilimanjaro stars wakipangwa na Ethiopia sambamba na Zambia ndugu zao Zanzibar Heroes wamewekwa katika kundi C pamoja na Sudan na Rwanda.

Makundi Kamili:


Kundi A: Ethiopia, Zambia, Tanzania, Somalia

Kundi B: Kenya, Uganda, Burundi, Djibouti.

Kundi C: Sudan, Rwanda, Sudani Kusini, Zanzibar.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.