CHAMA cha soka Zanzibar (ZFA ) kimethibitisha kuwa Zanzibar itakuwa mwenyeji wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’ Julai mwakani.
Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa chama hicho, Masoud Attai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana.
“Ni kweli Zanzibar imepeleka maombi CECAFA (Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati) kuandaa michuano hiyo tumekubaliwa na kilichobakia ni kuona kwamba tunaandaa mashindano hayo, “ alisema.
Aidha alisema kuwa tayari wameshapeleka barua Baraza la Taifa la Michezo la Zanzibar (BTMZ ), na tayari wameshawajibu barua hiyo na kilichobakia ni mipango ya pamoja kati yao na viongozi wa BTMZ, ili kupanga programu ya kucheza michuano hiyo.
Attai alisema kwa mujibu wa programu yao viwanja vitakavyotumika ni vya Gombani Pemba na Amani Zanzibar kama hali itaruhusu.
Chanzo: Habari leo
0 comments:
Post a Comment