simba

AWADHI JUMA AIOKOA SIMBA KWENYE DHAHAMA YA KICHAPO, WAAMBULIA SARE MBELE YA JAMHURI


Magoli mawili ya kiungo wa Simba SC anaetokea visiwani Zanzibar Awadh Juma imeiondolia aibu ya kichapo Simba SC katika mchezo wake wa kwanza wa kombe la mapinduzi dhidi ya Jamhuri ya Pemba.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Amani, ulianza kwa kasi na kuashiria kuwa kungetokea magoli mengi zaidi katika mchezo huo kutokana na makosa ya mabeki ya kila upande waliyokuwa wanayafanya.

Kama safu ya ushambuliaji ya Jamhuri ya pemba ingeongeza umakini zaidi basi wangeibuka na magoli hata manne sawasawa na simba sc ambapo safu ya ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa na Raphael Kiongera ilipoteza nafasi nyingi za kufunga katika mchezo huo.

Simba SC wakitokea kupoteza nafsi ya wazi ya kufnga goli Awadhi Juma aliiandikia Simba SC goli la kwanza katika dakika ya 12 ya mchezo.

Baada ya kuingia kwa goli hilo halikupoteza utulivu wa Jamhuri ya Pemba, na katika dakika ya 16 Mwalim Mohammed Khamis aliisawazishia Jamhuri goli akimalizia kazi nzuri ya kiungo wa Jamhuri.

Baada ya kuingia goli hilo kulipelekea timu zote mbili kupoteza nafsi ya kujipatia goli la kuongeza na kupelekea dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Jamhuri walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Ammy Khamisi Bangaseka akimalizia kazi ya nzuri ya Mwalim Mohammed Khamisi.

Kuingia kwa goli hilo kulipelekea kocha kerr kuwanyanyua Mwinyi Kazimoto, Danny Lyanga, Ibrahim Ajibu na Hamisi Kiiza.

Mabadiliko yaliongeza kasi kwa upande wa simba sc na katika dakika ya 76 Awadhi Juma aliwasawazishia Simba SC goli la pili na kupelkea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.

Kwa matokeo hayo URA wanaongoza kundi A kwa kuwa na pointi 3 wakifuatiwa na Jamhuri na Simba SC katika pointi 1 huku JKU wakiwa wa mwisho bila pointi yoyote ile.

Kesho saa mbili usiku Yanga na Azam FC watakuwa na kibarua cha kuvuna point i3 watakapo kutana huku kukitanguliwa na mchezo kati ya Mafunzo na Mtibwa sugar.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.