Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Arusha (ARBA), Kipo katika hatua za mwisho kufanya uchaguzi Mkuu mapema mwezi huu uongozi utakao kiongoza chama hicho kwa muda wa Miaka Mitatu.
Mwenyekiti wa chama cha Mchezo wa Kikapu Mkoa wa Arusha (ARBA) Barick Kilimba alisema kuwa nafasi kuu mbili zitagombewa ikiwa pamoja na nafasi ya Mwenyekiti Mkuu, na Msaidizi wake, Katibu Mkuu na Makamu wake.
“Nilikuwa naongoza huku nacheza hivyo ilikuwa inaniwia vigumu sana wakati mwingine, katika kutoa maamuzi nilikuwa naogopa kuonekana napendelea Timu yangu, hivyo nimeamua niweke uongozi pembeni nibaki kuwa mchezaji pekee”
“Shida ilikuwa hakuna watu wa kuongoza nafasi hizi lakini tumewashawishi wale wachezaji wakongwe waje washike madaraka ili watuongoze na kutuonesha wao walikuwa Wanafanyaje kipindi wao wanacheza” Alisema Kilimba.
Aliongeza kuwa wanatarajia kufanya kikao cha viongozi wote Waliokuwa madarakani kwa sasa ili kupanga tarehe maalumu ya kufanya uchaguzi huo, ikiwa pamoja na kutangaza sifa za wagombea.
Pia ARBA Wanatarajia kuendesha Bonanza la mchezo huo kwa kushirikisha timu zote zinazopatikana Mkoani hapa pamoja na mikoa ya Jirani ikiwa na Lengo kupanua na kutangaza Mchezo huo katika ukanda wa Kusini.
Kilimba alisema kutoshirikiana baina ya viongozi ndio sababu kubwa ya Mchezo huo kufifia Mkoani hapa, kwa iongozi wengi kukwepa majukumu yao na kuwa Bize na mambo yao Binafsi.
Hata hivyo alikiri ARBA kukabiliwa na ukata kitu ambacho kilisababisha kushindwa kushiriki mashindano ya Kitaifa yaliyokuwa yanafanyika Mkoani Dodoma mwezi Disemba mwaka uliopita, licha ya kukiandaa kikosi.
0 comments:
Post a Comment