mtazamo

KWA MADUDU HAYA LIGI KUU INATOFAUTI GANI NA LIGI ZA MCHANGANI

Baada ya Tanzania kuchapwa goli 7 na Algeria ndugu zangu wa Sudani Kusini walikuwa wana nikejeli wakisema pamoja na uchanga wao hawa wezi kufungwa goli zote zile.

Wiki hii imeanza mambo ambayo ndugu zangu wa Sudan Kusini kama wangepata kukutana na mimi wakati wakiyafahamu matukio yaliyo tokea, wangeweza kunikejeli vibaya zaidikwa kuishusha hadhi ligi yetu kwa kuifananisha na ligi ya mchangani nchini mwao.

Unajua kwanini wangelisema hilo, ni ligi za mchangani pekee ndizo zinazo weza kupisha michuano maalum, isiyokuwepo kwenye kalenda ulimwenguni kote, ila kwetu Tanzania limewezekana kwa mara ya pili mfululizo.

Mwaka jana michezo ya Azam FC ilisogezwa mbele kupisha michuano maalum ambayo Azam FC ilialikwa nchini DRC Congo na mwaka huu teyari Azam FC wapo Zambia kwa ajili ya mwaliko wa michuano maalum, ila safari hii Simba na Yanga nao wameanza kujiandaa kutoka nche ya nchi huku ligi ikiendelea.

Ligi yenye wachezaji wanaolipwa mamilioni ya pesa kutoka pembe mbalimbali za Afrika, inasimama kupisha michuano maalum ambayo enzetu wanaitumia kama sehemu ya mwisho ya Pre season yao kwa kujianda kwa ajili ya ligi na michuano ya kimataifa.

Tumeapata kushuhudia hapa timu za Kenya, Uganda zikija kucheza na timu za Tanzania michezo ya kirafiki bila kuathiri ligi zao, ambazo wakati huo zikiwa zinaendelea, ila sisi tunaishusha hadhi ligi ambayo huenda ndiyo inayoangaliwa zaidia ukanda huu kwa ligi za ndani.

TFF mmeamua kuishusha hadhi ligi yetu, ambayo baadhi ya timu shiriki zilishaanza kunufaika kutoka kwa wadhamini wanaojitokeza, kutokana na hadhi ambayo ilikuwa teyari imeanza kujijengea lakini kwa sasa inaanza kushuka na hatimaye huenda kukapelekea kuipoteza wadhamini.

TFF msitufanye mashabiki wa soka kuendelea kujivunia na mafanikio ya Samata, badala ya kujivunia mafanikio ya soka kwa ujumla.

Kugharishwa kwa mchezo wa Tanzania Prisons dhidi ya Azam FC teyari ushaharibu program za mwalimu na uongozi mzima wa Prisons.

Baada ya mchezo wa leo Coastal union wananza maandalizi ya kucheza dhidi ya Yanga, na kama TFF watawakubalia yanga waende kuweka kambi Afrika kusini ina maanisha mchezo huo utaghaiurishwa na sijui nani ana beba gharama za kuaghirishwa mchezo huo.

Ni Tanzania pekee ambapo ligi kuu ya vodacom inasimama kupisha maandalizi ya michezo ya kimataifa, kupicha mashindano maalum.

Malinzi taratibu na TFF yako inanirudisha kule kwenye ile posti niliyo iweka kuwa sina imani na wewe pamoja na mpinzani wako wakati wa uchaguzi.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.