Unaweza sema mazoe hujenga tabia baada ya mtibwa sugar kucheza fainali yake ya tano ya kombe la mapinduzi na kutofanikiwa kutwaa kombe hilo mbele ya URA ya Uganda hii leo.
Katika mchezo huo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Amani hii leo URA waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 16 kupitia kwa Julius Ntambi goli lilo dumu kwa kipindi chote cha kwanza.
Katika kipindi cha kwanza URA waliuwanza mchezo kwa kujiami huku wakicheza soka la taratibu na pale walipoandika goli la kuongoza walidhibiti mianya yote ya kupitisha mpira katika eneo lao la ulinzi.
Mtibwa sugar wao waliuwanza mchezo kwa kufunguka kusaka goli la ushindi lakini walikosa mbinu ya kupenya ngome ya URA na kupelekea kwenda mapumziko wakiwa bado hawajapata goli.
Katika kipindi cha pili Mtibwa sugar wakicheza soka la kuvutia na kujaribu kutafuta goli la kusawazisha na kupelekea muda mwingi mpira kuchezwa katika eneo la URA na kadri dakika zilivyokuwa zinasogea ndivyo Mtibwa sugar walivyokuwa wana zidi kulisakama lango la URA.
Katika dakika ya 85 shambulio la kushtukiza linamkuta Peter Lwasa na kuipatia URA goli la pili akiwa ametokea benchi na dakika 3 mbele anaiandikia tena URA goli la tatu.
Japhari Salum alitumia ,makosa ya kipa wa URA kuiandikia Mtibwa sugar goli pekee katika mchezo huo katika dakika ya 90 na kupelekea mchezo kuimalizika kwa URA kuibuka na ushindi wa goli 3-1.
Kwa matokeo hayo URA wamekuwa mabingwa wa kombe la mapinduzi mwaka 2016 huku mshambuliaji wao Peter Lwasa akiibuka mfungaji bora wa michuano hayo yanayo fanyika kila mwaka.
HORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
Mwaka | Bingwa | Mshindi wa Pili |
---|---|---|
2007 | Yanga SC | Mtibwa Sugar |
2008 | Simba SC | Mtibwa Sugar |
2009 | Miembeni | KMKM |
2010 | Mtibwa Sugar | Ocean View |
2011 | Simba SC | Yanga SC |
2012 | Azam FC | Simba SC |
2013 | Azam FC | Tusker FC |
2014 | KCCA | Simba SC |
2015 | Simba SC | Mtibwa Sugar |
2016 | URA | Mtibwa Sugar |
0 comments:
Post a Comment