Wawakilishi wa Uganda katika kombe la Mapinduzi wamefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kufanikiwa kumaliza mchezo wao wa mwisho wa kundi A kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Jamhuri ya kisiwani Pemba.
Katika mchezo huo URA walianza mchaklato wa kusaka goli tokea katika dakika ya kwanza ya mchezo lakini mashambulizi yao yote yaliishia mikoni mwa kipa na mabeki wa Jamhuri na kupeleka mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili Jamhuri walianza kwa kulinda lango lao huku URA wakiongeza mashambulizi ambapo yalikuwa yana punguwa kulingana na dakika zilivyokuwa zinasogea na huku Jamhuri wakijaribu kupandisha timu.
Katika dakika ya 60 Kipa wa URA amanusura awazawadia goli Jamhuri baada ya kujaribu kumpiga chenga mshambuliaji wa Jamhuri na mshambuliaji huyo kuunasa mpira na kushindwa kuutia nyavuni.
Katika dakika ya 73 Jamhuri walipoteza nafasi ya kujiandikia goli la kuuongoza baada ya mshambulijai wao kubaki na kipa na kushindwa kuutia mpira nyavuni.
Dakika ya 74 hatimaye URA waliandika goli lao pekee la ushindi katika mchezo wa leo kupitia kwa Said Kyeyune kwa shuti alilopinga kwenye ukingo wa eneo la hatari na kutinga nyavuni.
Kuingia kwa goli hilo kuliwatuliza URA na kuanza kucheza soka la uhakika huku wakijaribu kulinda ushindi wao na kupelekea mchezo kumalizika kwa URA kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Kwa matokeo hayo URA anangoja mchezo wa mwisho wa kundi A kati ya Simba SC na JKU utakaochezwa usiku wa leo, ilikujua atakutana na nani katika hatua ya nusu fainali kati ya yanga na Mtibwa sugar.
0 comments:
Post a Comment