Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC wamemaliza wakiwa kinara wa kundi A baada ya leo kuifunga Mtibwa sugar goli 2-1 katika mchezo wa mwisho wa kundi B katika michuano ya kombe la Mapinduzi.
Katika mchezo wa leo Mtibwa sugar waliuanza mchezo kwa kasi na kuipelekea yanga ndani ya dakika 20 za mwanzo wakiwa hawajafanya shambulio lolote la maana katika lango la Mtibwa Sugar.
Mtibwa Sugar waliandika goli lao la kwanza kupitia kwa Ramadhan Shiza Kichuya katika dakika ya 10 akitumia vyema pasi ya Mzamiru Yassin na kuipa uongozi Mtibwa sugar.
Baada ya kuinmgia kwa goli hilo Yanga SC walianza kuutawala mchezo taratibu na kuanza kupeleka mashambulizi langoni mwa Mtibwa saugar.
Katika dakika ya 41 Issoufo Bobuckary aliiandikia Simba SC goli la kusawazisha kwa mpira wa adhabu aliopiga na kutinga nyavuni moja kwa moja na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.
Kipindi cha pili yanga SC walikianza taratibu huku wakiendelea kutawala mchezo na kadri dakika zilivyokuwa zinasogea walikuwa wanaongeza kasi ya mchezo.
Katika dakika ya 81 Malim Busungu aliandikia Yanga SC goli la pili akiunga kwa kichwa krosi ya Saimon Msuva na kupelekea mchezo kumalizika kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Katika mchezo wa leo Mtibwa sugar walimaliza wakiwa pungufu baada ya kiungo wake Henry Joseph kutolewa nnje kwa kadi nyekundu mara baada ya kunigia kuchua nafasi ya Ibrahim Jeba.
Kesho ndio hitimisho ya hatua ya makundi ambapo michezo ya mwisho ya kundi A itachezwa Simba SC wakiwa kabili JKU usiku na URA wakicheza dhidi ya Jamhuri saa 10 jioni.
0 comments:
Post a Comment