Mashindano hayo ya kufuzu kwa Olimpiki Kanda ya Afrika yatafanyika Yaounde, Cameroon kuanzia Machi 9 hadi 20, ambapo TBF inatarajia kupeleka timu iliyokamilika ya mabondia 10.
Alisema jumla ya mabondia 22, ambapo kila moja itakuwa na mabondia 11 wataunda timu ambazo zitakuwa chini ya makocha wanne.
Alisema kuwa kutakuwa na timu A na B, ambazo kila mmoja itakuwa na kocha mkuu na msaidizi wake kwa ajili ya kusaka mabondia 10 watakaoenda Cameroon kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ya mchujo.
Mwang’onda ambaye ni bondia wa zamani wa kimataifa wa Tanzania alisema mabondia hao walipatikana katika mashindano ya wazi ya taifa yaliyomalizika Ijumaa kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.
Katika mashindano hayo, mabondia wa Ngome waliibuka wa kwanza huku wakifuatiwa na JKT, Kigoma walishika nafasi ya tatu na Mwanza walimaliza wa nne.
Chanzo: Habari leo
0 comments:
Post a Comment