mingine

KATIBA ZA VYAMA VYA MICHEZO SERIKALI YA AGIZI ZIPITIWE


SERIKALI imeitaka Wizara ya Michezo na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia Katiba za vyama vyote na kuzikagua ili kuhakikisha zinaandaa sera ya michezo inayokwenda na wakati.

Hayo yalielezwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza na wadau na viongozi wa michezo nchini kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana.

“Katiba za vyama vingi vinawabeba waliopo madarakani, hivyo BMT inatakiwa kusimamia na kuondoa neno ridhaa na kuwa ya kulipwa, kwani michezo ni ajira,” alisema Majaliwa.

Pia Majaliwa aliagiza makocha wa michezo yote wasajiliwe na vyama vya michezo husika, huku akizitaka Halmashauri kuwa na bajeti za michezo na zitekelezwe.

Alihoji Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuiondoa ofisi ya Chama cha Makocha (Tafca) na kusema hata kocha wa timu ya vijana ya Taifa, Kim Poulsen ambaye amerejereshwa anatakiwa kusimamiwa na kukaguliwa na Tafca, huku akihoji sababu za TFF kumrejesha tena kocha wakati ndio walitangaza kumondoa.

Wadau kwa kushirikiana na wizara waandae sera ili baadaye itungwe sheria ambayo itaendana na michezo kwa wakati huo kwani iliyopo imepitwa na wakati, kwani ni ya 1967 na ilitungwa sheria kabla ya sera, jambo ambalo ni kinyume.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema kuwa sera ya michezo imepitwa na wakati kwani ilipitishwa na Bunge mwaka 1967, na kufanyiwa marekebisho 1971 na 1995 lakini bado inahitajika ipitiwe upya.

Majaliwa alijibu hoja za vyama vingi kuomba kujengewa viwanja vinavyohusika na michezo ya ndani na kusema serikali imepata mwekezaji kutoka Afrika Kusini, kampuni ya Bilioni Group ambao wameshatoa michoro ya namna uwekezaji wao utakavyokuwa ikiwamo bwawa la kuogelea, hosteli, maduka na ofisi za vyama vya michezo.

Chanzo: Habari leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.