CAF

MAFUNZO YAPOKEA MAFUNZO YA KUSAKATA SOKA TOKA KWA AS VITA

Mlinzi wa Mafunzo Abulhalim Abdalla (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka kiungo wa timu ya AS Vita Bernad Morrison katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Amani, Zanzibar jana. Mafunzo ilichapwa mabao 3-0. (Picha na Mwajuma Juma).
TIMU ya soka ya Mafunzo ya Zanzibar jana ilianza vibaya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa AS Vita ya Congo DR.

Tangu mwanzo wa kipindi cha kwanza cha mechi hiyo Mafunzo ilionekana kuelemewa karibu kila idara na kuruhusu wageni kutamba kana kwamba wanacheza nyumbani. Vita ilipata bao lake la kwanza katika dakika ya tano ya mchezo huo kupitia kwa Ikanga Mayimona baada ya kuunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Benard Morrison.

Mwamuzi wa mchezo huo aliamuru wageni wapige adhabu baada ya Emmanuel Ngudikana kuchezewa faulo na walinzi wa Mafunzo. Dakika ya 29 AS Vita walipata bao lingine mfungaji akiwa Ngudikana baada ya kuunganisha pasi ya Ngoda Muzinga na kuujaza mpira wavuni.

Dakika moja kabla ya kwenda mapumziko Muzinga aliifungia AS Vita bao la tatu. Dakika ya 79 wageni walipata penalti lakini mchezaji wake Benard Morrison alikosa baada ya kupiga mpira juu.

Chanzo: Habari leo

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.