simba

SIMBA, KIIZA WASHIKA USUKANI, NDANDA YAUA NANGWANDA


Simba SC sambamba na mshambuliaji wao toka nchini Uganda Hamisi Kiiza Diego wameshika usukani wa ligi kuu ya vodacom na ufungaji bora msimu huu, baada ya leo kuibuka na uashindi wa goli 2-1.

Simba SC leo walikuwa wageni wa Stand united katika uwanja wa CCM Kambarage na kufanikiwa kupata ushindsi wa 7 mfululizo chini ya kocha wao Salum Mayanja toka Uganda.

Simba SC waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 33 kupitia kwa Amisi Kiiza goli lilo wapeleka mapumziklo wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha pili Kiiza aliifungia Simba SC goli la pili likiwa ni goli lake la 16 katika msimu huu katika dakika ya 47, na goli hilo linamfanya Kiiza kuwa kileleni kwa zaidi ya magoli mawili mbele ya mshindani mwqenzake Amisi Tambwe mwenye magoli 14..

Stand united walipata goli lao la kufutia machozi kipindi cha pili na kupeleka mchezo kumalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindsi wa goli 2-1 na kuifanya Simba SC kukaaa kileleni kwa mara ya kwanza katika kipindi hiki cha miaka mitatu.

Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja wa Nangwanda sijaona Ndanda FC wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 mbele ya Majimaji FC.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.