yanga

Yanga yaondoshwa Urafiki


Kikosi cha Yanga kilicho cheza dhidi ya Zamalek

Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Dar Young Africans 'Yanga' wameondolewa katika michuano ya kombe la Urafiki inayohusisha timu za Tanzania Bara na zile za visiwani Zanzibar inayoendelea Visiwani humo.

Yanga imetolewa katika mashindano hayo na wandaaji wa michuano hiyo (chama cha soka Zanzibar (ZFA) na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar) kwa kitendo cha timu hiyo kupeleka kikosi B badala ya cha kwanza, ambacho kilipokea kichapo cha goli 3-2 toka kwa Jamhuri ya Pemba hapo jana.

Kwa kitendo hicho cha yanga kurejeshwa jijini Dar es salaam kunapelekea kundi B kubakikiwa na timu tatu ambazo ni Jamhuri, Falcon na All Stars.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.