ASFC

SIMBA YAIADHIBU SINGIDA UNITED GOLI 5-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI


Simba sc wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la TFF linalo dhaminiwa na Azam TV kupitia Azam Sports HD, baada ya kuichapa Singida United goli 5-1.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa Simba SC waliuwanza mchezo kwa kasi ya chini na Singida United ndio walikuwa wa mwanzo kufika katika robo ya wapinzani wao, kabla ya Simba SC kujibu mapigo katika dakika ya 2 na kufanikiwa kupata faulo.

Uokoaji wa faulo hiyo iliyopigwa na Brian Majegwa na kumkuta Danny Lyanga aliyeipiga shuti kali lililo tiwa kimiani na beki wa Singida united katika harakati ya kuokoa mpira huo na kuiandikia Simba goli la kuongoza.

Kuingia kwa goli hilo kuliongeza kasi ya Simba SC na kuanza kutawala mchezo huku Singida united wakifanya kazi ya ziada ya kuoka hatari langoni mwao .

Katika dakika 19 Hamisi Kiiza aliiandikia Simba SC goli la pili baada ya Singida united kwenda kusaka goli la kusawazisha, na kuruhusu mwanya ambao Simba SC waliutumia vyema kuandika goli la pili.

Kuingi kwa goli hilo Simba SC waliendeleza kuishambulia Singida united lakini umakini wa kipa wa Singida united na beki wake, ilipelekea mchezo kwenda mapumziko kwa Simba SC kuwambel kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili Singida United walikianza vyema na kuhatarisha usalama wa simba sc, kama safu yake ya ushambuliaji ingekuwa vyema ingeweza kupata goli katika dakika 10 za mwanzo wa kipindi cha pili.

Alikuwa Hamisi Kiiza aliyeirejesha Simba SC katika utawala wa Mchezo baada ya kupata goli la 3 katika dakika ya 66 ya mchezo akimalzia krosi ya Brian Majegwa.

Kuingia kwa goli ilo kuliwapoteza Singida united na kupeleka Simba SC kutawla mchezo na kucheza watakavyo.

Katika dakika ya 84 Awadh Juma aliiandikia Simba SC goli la 4 kabla ya kuandikia goli la 5 katika dakika ya 88.

Kuingia kwa magoli hayo mawili ya Awadhi Juma kuliwafanya Simba SC kupoteza umakini katika safu yao ya ulinzi na kama Singida united wanguekuwa makini wangeandika goli 2 katika dakika hizo za mwisho.

Paulo Malama aliiandikia goli la kufutia machozi Singida united katika dakika 2 za nyongeza kwa shuti kali la mita 25 na kupeleka mchezo kumalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 5-1.

Kwa matokeo hayo Simba SC wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayotoa timu itakayo iwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho la CAF mwakani.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.