ASFC

WAWA AIFUNGIA AZAM FC GOLI MUHIMU HII LEO, NA KUIPELEKA ROBO FAINALI

Beki wa Azam FC kutoka nchini Ivory coast Pascla Wawa hii leo ameifuniga Azam FC goli lake la kwanza katika mashindano toka ajiunge na mabingwa hao wa Afrika Mashariki na kati.

Goli la Wawa hii leo lilikuwa la kusawzaisha katika mchezo wa kombe la TFF linalodhaminiwa na Azam TV kupitia Azam Sports HD, dhidi ya Panone mchezo uliochezwa katika uwanja wa Ushiriki mkoani Kilimanjaro na kupeleka Azam FC kuwa timu ya mwishho kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Katika MChezo wa leo Azam FC waliuwanza taratibu, huku Panone wakionekana kutojiamini katika dakika 10 za mwanzo wa mchezo.

Katika kipindi cha kwanza Panone walionekana kuwa hatari zaidi ya Azam FC na walionekana kucheza vyema katika eneo la kati, huku Azam FC wakicheza mipira mirefu isiyokuwa na faida.

Katika kipindi hicho cha kwanza Azam FC walipoteza nafasi moja kupitia kwa Allan Wanga aliyeshindwa kuunga krosi maridhaa ya Faridi Mussa Malik na huku Panoni nao wakipoteza nafasi moja.

Hadi timu zinakwenda mapumziko hakuna timu iliyo ona nyavu za wapnzani wao, na katika kipindi cha Azam FC walianza kwa mabadiliko mawili ambapo alimpumzisha Dider Kavumbagu na Ame Ally na nafasi zao zikachukuliwa na Salum Abubakari na Kipre Tcheche.

Mabadiliko hayo yalirejesha uhai katika eneo la kati la Azam FC, ambapo walirejesha utawala katika himaya yao, huku Panone FC wakitumia mipira ya kushtukiza.

Katika dakika ya 48 Panone FC waliandika goli la kuongoza kupitia kwa Geodfrey Buda akiiunga mpira wa adhabu faulo kwa kichwa na kuipa uongozi Panone.

Kuingia kwa goli hilo kulipeleka Panone kubakisha mshambuliaji mmoja na kujazana katika kati ya uwanja ambapo Azam FC muda mwingi walikuwa katika eneo la Panone.

Katika dakika 57 Stewart Hall anamunigniza Jean Mugereneza kuchukuwa nafasi ya Franky Domayo mabadiliko yaliyoongeza ufanisi katika kuipandisha timu mbele.

Dakika ya 63 Pascal Wawa anaisawazishia Azam FC kwa kichwa akiunga kona ya Erasto Nyoni na kuwafanya Panone FC nao kujaribu kufunguka kusaka goli la kuongoza.

Dakika ya 77 makosa ya mabeki ya Panone kushindwa kuoka mpira wa kona uliopigwa na Erasto Nyoni unamfanya Allan Wanga kuipasia nyavu na kuiandikia Azam FC goli la pili goli liliodumu mpaka mwisho wa mchezo.

Kwa matokeo hayo ya ushindi wa goli 2-1, Azam FC wanaungana na Yanga SC, Simba SC, Mwadui FC, Ndanda FC, Coastal Union, Tanzania Prisons na Geita gold katika hatua ya robo fainali itakayo chezwa mwezi ujao katika viwanja vinne.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.