CAF

YANGA WAANZA KUTOA DOZI KLABU BINGWA AFRIKA


Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga SC wameanza vyema michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya leo kuibua na ushindi wa goli 1-0 toka kwa Cercle de Joachim ya Mauritius.

Katika mchezo huo uliofanyika nchini Mauritius, Yanga waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 17 kupitia kwa Donald Ngoma, goli lililodumu dakika zote tisini.

Yanga SC ambao waliingia nchini Mauritus jana usiku wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0, katika mchezo huo wa awali, ambapo watarejeana wiki mbili zijazo jijini Dar es salaam.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.