ASFC

KAPOMBE AIPELEKA AZAM FC NUSU FAINALI, WAKIICHAPA GOLI 3 PRISONS


Magoli ya beki wa kimataifa wa Tanzania Shomari Kapombe yameipeleka Azam FC katika hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho la soka nchini TFF linalo dhamniwa na Azam TV kupitia Azam Sports HD.

Azam FC hii leo walikuwa wenyeji wa Tanzania Prisons katika mchezo wa robo fainali ya kombe la TFF na dakika 90 zilimalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 3-1.

Alikuwa Shomari Kapombe aliiandikia Azam FC goli la kwanza katika dakika ya 9 akimaliza mpira ulioshindwa kuokolewa vyema na mabeki wa Tanzania Prisons.

Kuingia kwa goli ilo kuliwapa utawala wa mchezo Azam FC na kuziba mianya ya Tanzania prisons kupitisha mpira na kuamua kuanza kutumia mipira mirefu.

Katika dakika ya 31 Jeremia Juma aliisawazishia Tanzania Prisons na kupeleka mchezo kwenda mapumziko wa wakiwa sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kila timu ikishambuliana kwa zamu, na katika dakika ya 50 Shomari Kapombe aliindikia Azam FC goli la pili na katika dakika ya 63 kocha Stewart Hall ambaye hakuwa na mipangu ya kumtumia kabisa katika mchezo wa leo alimpumzisha na kuingia Farid Mussa.

Azam waliandika goli lao la tatu kupitia kwa mtokea benchi Khamis Mcha Viali aliyeingia kuchukuwa nafasi ya John Bocco katika dakika ya 86 na kupeleka mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 3-1.

Kwa matokeo hayo Azam FC wameungana na MWadui FC katika hatua ya nusu fainali ya michunao hiyo ya kombe la TFF.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.