Abdillahie ambaye pia anajulikana kama Adi, anacheza Mansfield inayoshiriki Ligi Daraja la Pili England, amesema amefurahi kuona anaungana na wachezaji wengine kuitumikia nchi yake na kuahidi kutoa ushirikiano.
“Nafurahi kuichezea nchi yangu, hivyo sitawaangusha Watanzania, endapo nitapata nafasi ya kucheza ila joto linanipa shida kidogo, lakini nitazoea,” alisema.
Alisema amezaliwa Tanzania na baadae wazazi wake walihamia Uingereza, ambako ndiko alikokulia, pia amefurahi kukutana na Mbwana Samatta mchezaji ambaye ameing’arisha Tanzania baada ya kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika.
Naye Mshauri wa Benchi la Ufundi la Taifa Stars, Abdallah Kibadeni amesifu kiwango cha mshambuliaji huyo na kudai ataisaidia timu.
“Kwa muda mchache niliomwona nimeridhika na kiwango chake na naamini ataweza kuisaidia timu na nchi kwa ujumla,” alisema Kibadeni.
Adi ambaye anacheza namba tisa, alizaliwa Februari 20, 1992 na alianza kucheza soka akiwa kwenye Akademi ya Leicester City 2008-2011, 2011-2013 alicheza Burton Albion, 2013-2014 alikuwa Lincolin City na 2014 -2015 Oxford City.
Chanzo: habari leo
0 comments:
Post a Comment