ASFC

MWADUI WAICHAPA GEITA GOLD GOLI 3-0, "MWENYE NACHO HUZIDISHIWA" JULIO

Kabla ya mchezo wa robo fainali ya kombe la TFF linalodhamniwa na Azam TV, kati ya Mwadui FC na Geita Gold, kocha wa Mwadui alitoa kauli ya kwamba mwenye nacho hozidishwa, ndisho kilichotokea baada ya mchezo kumalizika ambapo Mwadui FC iliibuka na ushindi wa goli 3-0.

Katika mchezo huo Geita gold alianza kwa kasi na kutengeneza nafasi za kufunga goli ambazo walishindwa kuzitumia.

Vijana wa Julio walianza taratibu na kadri muda ulivyosogea kasi yao ilikuwa inaongezeka huku vijana wa Matola Geita Gold Stars wakipoteza umakini katika nafasi ya ulinzi na nafasi ya ushambuliaji.

Alikuwa beki Jerum Mugeveke aliiandikai Mwadui FC goli lake la kwanza katika dakika ya 23, na dakika mbili mbele Jerry Tegete aliiandikia Mwadui goli la pili akiunga kwa kifua mpira wa adhabu uliopigwa na Athuman Iddi Chuji.

Kuingi kwa magoli hayo ndani ya dakika mbili kulipeleka kwa Mwadui Fc kupunguza kasi na kuendelea kutawala mchezo, na huku Geita wakiendelea kusaka goli.

Kipindi cha pili Mwaduid FC waliendelea na mchezo wao wa taratibu na kutibua mipango ya Geita gold.

Katika dakika ya 56 Mwadui FC waliandika goli la tatu kupitia kwa Jabiri Azizi akiunga pasi ya David Luhende na kuplekea mchezo kumalizika kwa Mwadui Kuibuka na ushindi wa goli 3-0.

Mwadui FC wanakuwa timu ya kwanza kutingas nusu fainali ya kombe la TFF, ambapo michezo ya nusu itachezwa mwishoni mwa mwezi wa 4, huku ratiba ya michezo ya hiyo kutolewa aprili 7 ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo wa mwisho wa robo fainali kati ya Simba SC na Coastal union.

Michezo mingine ya robo fainali itachezwa marchi 31 ambapo Azam FC watacheza na Prisons, Yanga wakicheza na Ndanda FC.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.